Beyonce na Papa ni miongoni mwa waliopoteza tiki za bluu katika Twitter

Beyonce na Papa ni miongoni mwa waliopoteza tiki za bluu katika Twitter

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Kuanzia leo, akaunti zao za Twitter hazijathibitishwa tena.

Kampuni hiyo kubwa ya mitandao ya kijamii ilianza kuondoa uthibitishaji wa tiki ya bluu uliokuwa ukitamaniwa kutoka kwa maelfu ya akaunti kuanzia siku ya Alhamisi.

Hatua hiyo inajiri huku mmiliki wake Elon Musk akijaribu kubadilisha kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii ili kupata faida. Watumiaji wanaotaka kuhifadhi tiki za bluu za majina yao lazima walipe $84 kwa mwaka (£67) ili kujisajili kwenye Twitter Blue.

Mabadiliko yalipotokea, wengi waliothibitishwa hapo awali walienda kwenye kurasa ya Twitter kufanya utani kuhusu hilo, au kueleza hasara walizopata.

Mwana Olimpiki wa Marekani Lolo Jones alibainisha kuwa bado amethibitishwa pale inapozingatiwa: wasifu wake wa mahusiano.

Watumiaji wengine walisema kwa kejeli kwamba muigizaji Jason Sudeikis alipoteza uthibitishaji wake, wakati Ted Lasso, hajapoteza.

BBC
 
Twitter imeanza kuondoa alama ya tiki ya bluu kutoka kwa watumiaji wasiolipa

Watu mashuhuri kama Beyonce, Cristiano Ronaldo, Papa Francis, Bill Gates, Diamond Platnumz, Ali Kiba, Davido, Wizikid, Burna Boy na wengine wengi wamepoteza alama ya bluu katika mtandao huo
 
Ya Mwigulu uliicheki?

Huyu amezoea kutukata, nataka nione wakimkata yeye reaction yake inakuwaje
 
Twitter imeanza kuondoa alama ya tiki ya bluu kutoka kwa watumiaji wasiolipa

Watu mashuhuri kama Beyonce, Cristiano Ronaldo, Papa Francis, Bill Gates, Diamond Platnumz, Ali Kiba, Davido, Wizikid, Burna Boy na wengine wengi wamepoteza alama ya bluu katika mtandao huo
Wote uliowataja bado wanazo
 
Kulipia na kuwa na blue tick kuna faida kubwa kwao kuliko kutolipia....Watatokea Ma Parodies kibao hivyo watu sahihi wataogopa kufanya nao biashara hao watu.
 
Back
Top Bottom