Bi harusi aingia mitini lakini sherehe yaendelea

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325
UPDATE

Mila na desturi kisa cha harusi kutofungwa

Hii ni update kuhusu yule Bi harusi aliyeingia mitini. Chanzo cha harusi kutofungwa kilitokana na kutokuwa na mawasiliano mazuri na washenga wake ambao ni Bwana Amoni Mwangosi ambaye ni mshenga wa Bibi harusi na Bwana Angolile Mwakisilwa ambaye ni mshenga kwa upande wake wa Bwana harusi.

Bwana harusi alitumia watu wengine kupeleka nauli ya Sh. 24,000/= ya kumchukua bi harusi na mpambe wake bila kufuata taratibu za kimira za kuwajulisha washenga wake ndiyo waende kumchukua mchumba wake hata hiyo watu hao walikataliwa kwa kutotambuliwa na familia hiyo ya bi harusi na kutaka wahusika wafike ili wakabidhiane kwa taratibu zinazotambulikana.

Kwa upande wake wa Mzazi wa Bibi harusi Mzee Akimu Mwalukosya, amesema hana kinyongo bali yaliyopita si ndwele na wagange yajayo kwani makosa yaliyofanyika yanazungumzika.

Jana (Jumanne) jioni kamati ya maandalizi upande wa bwana harusi walikutana kujadili suala hilo. Hata hivyo kamati ya sherehe ya bwana harusi itakutana leo (Jumatano) kupata hatima ya harusi hiyo.

Bi harusi wakiwa na mama yake



Wakati wakichumbiana




Hii ni kwa mujibu wa blogu ya Mbeya Yetu. Jana Bi harusi mmoja aliingia mitini; hakutokea kabisa kanisani wala kwenye ukumbi wa sherehe. Wanakamati walishikwa na butwaa huku wengine wakilia. Licha ya Bi harusi kuingia mitini, sherehe iliendelea kama kawaida ukumbini jana usiku. Bwana harusi alishindwa kuja ukumbini kwa machungu aliyokuwa nayo. Kwa mujibu wa blogu hiyo sababu ya Bi harusi kuingia mitini bado haijafahamika. Sikupenda kuweka picha lakini kwa vile leo ni April fool watu wasingeamini hii habari.

Maandalizi ya ukumbi wa harusi kama yalivyokuwa yanaonekana jana.



Wanakamati wa harusi baada ya kupewa taarifa yakuingia Bi harusi kuingia mitini. Baadhi yao waliangua kilio ukumbini hapo.



Wazazi wa bwana harusi wakishuusha maombi ukumbini hapo.



Wazazi na ndugu wa bwana harusi wakiwa mbele ya wageni waalikwa.



Dada za bwana harusi pamoja na wazazi wakipokea zawadi kwa niaba ya bwana harusi ambaye naye alishindwa kuja ukumbini kwa machungu aliyokuwanayo



Baadhi ya waalikwa wakiwa haamini kilichotokea



Mama mzazi wa bwana harusi akitambulishwa bila kuwepo kwa maharusi.



Kwa picha na habari zaidi tembelea blog ya Mbeya yetu: Mbeya Yetu
 
Unajua haya mambo ya watu kuingia mitini siku ya mwisho huwa yanatokea na mara nyingi sababu huwa ni usaliti wa dakika za mwisho na mtu anaona kuliko kufunga ndoa na kuishi na mtu wa namna hiyo bora asifunge kabisa.

Mfano - mtu unakuta wakati anajiiandaa kufunga ndoa kesho leo anaenda kufanya mampenzi na mpenzi wake wa zamani ambae anampenda - eti wenyewe huwa wanasema wanaagana kimapenzi!

Sasa ikitokea mtu anagundua kuwa kafanyiwa usaliti basi anaamua asifunge harusi yenyewe kabisa.

Kama wanafanya mapenzi siku moja kabla ya ndoa au siku ya ndoa kabisa kwanini anataka kuoa/kuolewa na mtu mwingine? - ndio maana watu huingia mitini!
 
Reactions: EMT
.....akunyimae kunde.....

Kwa eksipirensi yangu kuhusu ndoa, heri ya hiyo nusu shari....
bwana harusi usomapo msg hii, kumbuka "likuepukalo lina heri nawe!"
bwana asifiwe!

Ameen!
 

Ndio maana siku yangu yakuoa,sitofanya sherehe yeyote.Harusi msikitini.
 
mambo mengine utadhani maigizo yaani.. unaweza kukuta bi harusi kafichwa sehemu na kiboifrendi chake
 
Kila jambo lina maana yake,bwn harus asonge mbele
 
Sasa hiyo sherehe ina muhimu gani ikiwa wahusika hawapo for whatever reason. Na mama anatambulishwa kama nani, vitu vyengine ni ujinga mtupu. Wangekaa nyumbani kumfariji aliyetemwa na hii ni aibu kwa family zote mbili husika.
 
pole ndugu kwa yote. bali mungu mkubwa mshukuru kwa kila jambo.
 
sherehe lazima ifanyike kwa kuwa watu walishachangishwa.
 
Labda ana wenyewe......................kheri nusu ya shari kulikoni shari kamili...........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…