Bi harusi aliyetoroka apatikana

Bi harusi aliyetoroka apatikana

Mavindozii

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2012
Posts
2,111
Reaction score
2,781
Ni yule Bi harusi aliyetoroka akiwa saloon sasa amepatikana mkoani Arusha, na hali yake haikuwa nzuri alikuwa anaweweseka, habari zinadi kwamba anapatiwa matibabu Selian hospital, Doroth Msuya ( Kulia )

Moshi. Bibi harusi Doroth Msuya aliyetoroka saluni akipambwa saa tatu kabla ya kufungwa kwa harusi yao na kumwacha solemba bwana harusi, Joseph Machange amepatikana jijini Arusha.

Polisi mkoani Kilimanjaro imesema binti huyo hakutekwa nyara kama ambavyo wanafamilia walitoa taarifa Kituo cha Polisi Himo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani alisema jana kuwa uchunguzi uliofanywa umethibitisha kuwa bibi harusi huyo hakuwa ametekwa nyara. Polisi walifungua jalada la uchunguzi na ilibainika kuwa taarifa za kutekwa zilizokuwa zimetolewa hazikuwa na ukweli, bali aliondoka kwa kupanda pikipiki, alisema.

Kamanda Ngonyani alisema uchunguzi huo ulibaini kuwa wakati akipambwa, aliomba kwenda kujisaidia na baadaye kuomba apelekewe kanga na tishu lakini akatumia mwanya huo kuondoka, alisema.

Alisema uchunguzi huo umebaini kuwa baada ya kupanda pikipiki ilimpeleka hadi kituo cha mabasi na alimlipa dereva wa bodaboda kisha alipanda gari la abiria lililompeleka hadi mjini Moshi.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita saa 6.30 mchana eneo la Lole huko Mwika, Moshi wakati bibi harusi huyo alipotoroka saluni akimwacha mpambe wake akiendelea kupambwa.

Ndoa hiyo ilikuwa ifungwe saa tisa alasiri katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Lole Dayosisi ya Kaskazini na baadaye sherehe ingefanyika katika Ukumbi wa Mamba Complex.

Habari zilizopatikana jana kutoka kwa familia ya Machange, zilieleza kuwa Doroth alipatikana juzi baada ya kuonekana akiweweseka, kisha akapelekwa hospitali ya Seliani kwa matibabu.

Ndugu wa karibu wa familia ya Machange ambaye aliomba jina lake lisitajwe, alisema kulikuwa na kikao kilichokuwa kikiendelea kati ya familia ya Machange na Msuya.

Jana (juzi) tulipigiwa simu na kuelezwa kuwa Doroth amepatikana Arusha lakini yuko kama hajielewielewi na hajui nini kimetokea, Alisema.

Habari zaidi kutoka ndani ya familia hiyo, zinadai kuwa bibi harusi huyo alikuwa ametaka harusi hiyo iahirishwe na ombi hilo alilitoa zaidi ya mara 10 bila kueleza sababu.
 
Humu ndani kama sijakosea kuna mdada alisema inawezekana huyu bibi harusi alitupiwa jini.
 
Isije ikawa:
1. malaria imepanda kwa kichwa

2. Sayansi ya kiafrika imetumika.... hapo bwana harusi abanwe na ahojiwe vizuri alimmwaga nani ili amuoe huyo
 
Hyo n sayansi ya kiafrica inasemekna bwana harusi alishawah ishi na mwanamke na kamzalsha wstoto wawili....
 
Mmmmh kwaiyo alivyopanda gari la abilia kuelekea mosh mjini alikuwa bado amevaa shela???
 
Huyo bibi harusi ananipa impression ya double dealer.Si ajabu
alikuwa na mwanaume mwingine walioahidiana kuoana na alipoona familia
ya Machange inaharakisha harusi, mdada kachanganyikiwa!
 
Simpo, hamna ndoa hapo na huyo bi harusi alikuwa analazimishwa kuolewa!
 
Habari zaidi kutoka ndani ya familia hiyo, zinadai kuwa bibi harusi huyo alikuwa ametaka harusi hiyo iahirishwe na ombi hilo alilitoa zaidi ya mara 10 bila kueleza sababu.[/QUOTE]

Nahisi tatizo lipo hapa zaidi
 
Habari zaidi kutoka ndani ya familia hiyo, zinadai kuwa bibi harusi huyo alikuwa ametaka harusi hiyo iahirishwe na ombi hilo alilitoa zaidi ya mara 10 bila kueleza sababu.

Nahisi tatizo lipo hapa zaidi[/QUOTE]

exactly! mzizi wa tatizo upo hapa.
 
Kweli mkuu, haiwezekani mtu atake kuahirisha ndoa bila sababu. Kuna kitu hapo nyuma

ningekua mimi akiomba tuahirishe mara moja ndo naahirisha mazima 🙂[/QUOTE]
Hahhaha wewe nawe mtata sasa. Inategemea na sababu ya kuahirisha kama ikiwa na uzito kwenu wote wawili
 
Pole yake, Bwana Harusi ajibu mashitaka maana anajua tatizo.

na nyie wanaume muwage mnasema ukweli ili sisi tuwe huru.
 
Isije ikawa:
1. malaria imepanda kwa kichwa

2. Sayansi ya kiafrika imetumika.... hapo bwana harusi abanwe na ahojiwe vizuri alimmwaga nani ili amuoe huyo
Na huyo demu nae abanwe,alikula vya nani alafu akakimbilia kwa bwana mwingine?
 
Anashindwa kumwambia ukweli mshikaji hampendi na mshikaji anashindwa kuona kuwa binti hamtaki...akubali tu binti hamtaki basi
 
Back
Top Bottom