Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Bi. Khadija Nkomanile ndiye mwanamke pekee aliyenyongwa na Wajerumani kwa kushiriki wake katika vita vya Maji Maji (1905 - 1907).
Wakati tunawaadhimisha wanawake ni muhimu tukamkumbuka mama yetu huyu ambae jina lake lipo pamoja na majemadari wanaume 62 walionyongwa na kuzikwa kwenye kaburi la halaiki.
Majemadari hawa wa Vita Vya Maji wote wamelala ndani ya kaburi moja ila Nduna Abdulrauf Songea Mbano yeye kazikwa kaburi la peke yake pembeni.
Picha: Katika hao waliosimama wa kwanza kulia ni Nduna Abdulrauf Songea Mbano.
Bahati mbaya sana wanahistoria hukwepa kuwataja mashujaa hawa kwa majina yao ya Kiislam mfano wa Khadija Mkomanile au Abdulrauf Songea Mbano.
Nimemuuliza Mwalimu Hussein Bashir ambae ameandika kitabu, ''Jihadi Kuu ya Maji Maji,'' ambacho ni kitabu kizuri sana kuhusu Vita Vya Maji Maji na yeye akanigusia kidogo tu kuhusu Bi. Khadija Mkomanile kama anavyozungumza hapo kwenye hiyo video.
Soma barua ya Chifu Songea bin Ruuf kwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:
''Asalaam Aleikum, Ninakuletea barua kupitia Kazembe.
Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini.
Tupo katika kupigananao hapa.
Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano.
Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea.
Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).
Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu.
Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa.
Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe.
Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.
Chupa hii, na daíwa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita. Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.
Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.
Hassan bin Ismail anakusalimu.
Salam nyingi,
Sultan Songea bin Ruuf.''