Bi. Khadija Mkomanile, mwanamke jasiri wa Vita vya Maji Maji

Asante sana kwa historia japo ni fupi ila kuna kitu nimejifunza
 
Sema historia yetu inawatenga sana wanawake hata Bibi Titi historia ya ukombozi wa Nchi haimuongelei kabsa lkn ni katika wanawake waliokua mstari wa mbele kwenye ukombozi wa taifa letu dhidi ya mkoloni..
 
Lengo lako ni moja tu!
Kutuambia mashujaa waliopigana vita vya majimaji ni waislamu na unataka kutuambia kuwa historia imewatenga.
Mzee kwa Udini hujambo.
Itabidi ugombee urais kupitia NRA ama ACT/CUF na uchaguliwe tuone utatufikisha wapi kama watanzania.

Sijui utaisilimisha nchi yote ama lah!
 
MKOMANILE: MWANAMKE SHUJAA WA VITA VYA MAJIMAJI.

Na mwandishi Francis Daudi

Kwa kipindi kirefu wanawake wa Afrika wamekuwa begabega na wanaume katika harakati mbalimbali za kulikomboa bara letu, lakini katika makala, vitabu, majarida ya kisiasa na hata ya kihistoria yamekuwa hayawapi nafasi ‘mashujaa wanawake’.

Wakati wa vita vya kizalendo vya Majimaji 1905 -1907 vilivyoongozwa na watanganyika wa makabila mbalimbali dhidi ya wakoloni wa kijerumani ‘wadachi’ wanawake walijitoa ili kupinga udhalimu wa wakoloni.

Vita vya Majimaji viliunganisha makabila ya wamakonde,wangoni,wangindo, wamwera,wabena, wamatumbi, wapogoro,wambunga, wazaramo na makabila mengine madogo madogo kati ya mwaka 1905 mpaka 1907. Ingawa mwisho wa harakati hizi waafrika walishindwa vibaya na majeshi ya Wadachi lakini kwa watanganyika yalikuwa ni mwanzo wa mapambano ya kutaka kujitawala katika nchi yetu.

Tarehe 27, Februari 1906 ni siku ambayo baadhi ya viongozi wa vita hivi walinyongwa mpaka kufa mjini Songea mbele ya ndugu zao. Kati ya walionyongwa ni mwanamke mmoja tu mzalendo na shujaa aliyeogopwa na wadachi kwa kuwezesha kufanikiwa kwa mapambano katika jamii ya wangoni.

Nkomanile, Mkomanile au Nkomandire ni mwanamke pekee aliyenyongwa siku nyeusi katika historia ya wangoni, maandishi na masimulizi mbalimbali yanatumia majina hayo yakimaanisha mtu mmoja.

Hakuna maandishi au masimulizi ya kutosha ya kihistoria yanayohusu maisha ya utotoni ya Mkomanile, katika utangulizi wa kitabu cha ‘Utenzi wa vita vya Majimaji’ kilichoandikwa na Abdul Karim bin Jamaliddini ulioandikwa na Bi Margareth Bates anaeleza kuwa Omari Kinjala alitumwa Ungoni( maeneo ya sasa ya Songea) toka Liwale akifuatana na mkewe ambaye Wadachi walimwita ‘Jumbess Mkomanire’ yaani Jumbe-wa- Kike, Mkomanire yeye alikuwa Mngoni jamaa wa Chabruma( Chifu wa Wangoni) huko Mashope.

Masimulizi na Maandishi yaliyopo yanapinga hilo kwani Nkomanile alikuwa Nduna wa Mashope na Kinjala hakuwahi kuwa mwenyeji wa Ungoni bali alitumwa tu toka Liwale kupeleka ujumbe wa vita vya Majimaji.

Kitabu cha ‘The Majimaji War in Ungoni’ yaani ‘Vita vya Majimaji katika Ungoni’ kilichoandikwa Mapunda O.B na Mpangala G.P wanaeleza kuwa Omari Kinjala alitoka Liwale na alipoingia maeneo ya Wangoni hasa Mshope yaliyokuwa chini ya Nkosi Chabruma alishindwa kufikisha ujumbe kwa mtawala(Chabruma).

Hivyo aliwasiliana na msaidizi wa kike wa Chabruma( kwa cheo cha Nduna) aliyejulikana kama Nkomanile. Inasemekana yule mgeni(Omari Kinjala) alianzisha mahusiano na Nkomanile hata siku moja usiku wakiwa kitandani Kinjala alitoboa siri ya nguvu ya maji na ujumbe aliotoka nao huko Liwale, Baadae walienda kumshawishi Chabruma kupokea maji na ujumbe wa vita dhidi ya wadachi ulioletwa. Hivyo ushawishi wa Nkomanile ndio hasa ulipelekea vita vya Majimaji kuingia rasmi katika jamii ya Wangoni kwa mara ya kwanza.

Inaelezwa kuwa baada ya Chabruma kupokea na kukubali ujumbe ule, Mkomanile alitumwa katika maeneo mbalimbali ya Ungoni kupeleka ujumbe wa mapambano dhidi ya ukandamizaji na uonevu uliofanywa na Wadachi.

Alitembea usiku na mchana kwenda tawala za mbalimbali ndani ya Ungoni; ili kurahisisha mapigano dhidi ya Wadachi, Mkomanile alitumika kuandaa vituo vine vilivyotoa ‘Dawa na Maji’ kwa wapiganaji toka eneo la Mshope lililokuwa chini ya Chifu Chabruma, Vituo hivyo inaelezwa kuwepo Namabengo, Lwegu, Uwereka(karibu na Gumbiro ya zamani) na Lukuyu ambapo palikuwa ni makao makuu ya Chifu Chabruma.
Mkomanile pia alipeleka taarifa toka kwa Chabruma kwenda kwa manduna(watawala waliokuwa chini ya Chifu Chabruma/ ni kama wasaidizi) na kwa machifu wengine waliokuwa na tawala zao, mfano Nkosi Mputa Gama wa Njelu. Ambapo Nkosi Mputa alifika na wapiganaji wake makao makuu ya Chifu Chabruma katika sherehe za unywaji wa Maji ili kujikinga na risasi za Wadachi wakati wa mapambano.

Masimulizi mengine yanamuelezea Mkomanile kama mwanamke aliyekuwa na nguvu kubwa ya uhamasishaji mapambano, ieleweke kuwa wapiganaji wa kiafrika katika Vita hivi walikuwa ni wanaume tu ambao walijifisha maporini na kuvamia Wadachi. Walitoka tu nyakati za Usiku na kufika vijijini kupata taarifa za Wadachi, baadae majeshi ya Wadachi yaligundua kuwa wanawake na vyakula vilivyokuwepo ndio viliwasaidia wapiganaji wa msituni kuendelea na Vita hivyo waliharibu mashamba na vyakula kwenye maghala. Hata hivyo Mkomanile aliweza kwenda kwenye maficho kuhamasisha na kupeleka siri za Wadachi bila kugundulika.

Bi Margareth Bates katika maelezo ya awali ya kitabu cha ‘Utenzi wa vita vya Majimaji’ anaeleza kuwa ‘yule mke wa kinjalla(Omari Kinjala) yaani Bi Mkomanire aliyehofiwa sana na Wadachi, mwishoni alikamatwa pia na kunyongwa kama walivyonyongwa wale viongozi wengine wa Maji Maji( au Hongo Hongo)’ hii inathibitisha kuwa Mkomanile alifanya kazi kubwa sana katika kuwezesha vita vya kuwakomboa Watanganyika wengine, huu ni ushujaa mkubwa na wa kuigwa na watanzania wa leo, Bila shaka hatuna tena vita vya kwenda msituni bali tunapaswa kusimama imara kupambana na Umasikini unaochangiwa hasa na rushwa, mikataba mibovu na uongozi mbaya.

Hadi mwisho wa Vita vya Majimaji katika jamii ya Wangoni, wanawake wengi walishiriki kwa namna moja ama ingine katika kusaidia harakati hizo ingawa jina la Mkomanile ndio linabaki kama alama ya uzalendo na ushujaa kwani alinyongwa tarehe 27, Februari 1906 na mashujaa wengine wa wanaume waliojitolea maisha yao ili kuondoa utawala wa kidachi.

Kwa kuhitimisha makala hii namnukuu msomi maarufu na mwandishi wa vitabu vya kiharakati Frantz Fanon katika kitabu chake kinachoitwa ‘Black Skin, White Masks’ anasema kwamba ‘Hoja sio kujua mambo ya ulimwengu bali kuyafanyia mabadiliko’ hivyo kwa sisi watanzania na waafrika kwa ujumla haitoshi tu kujua matatizo yanayotusumbua bali kupambana nayo na kuleta mabadiliko ya kweli.

Francis Daudi
+919513833624
 
Mohamed Said,

..kuna kisa cha kunyongwa kwa Selemani Mamba naomba ukitafute. kisa hicho nilikisoma zamani sana hata nimesahau jina la kitabu nilichosoma.
 
Kipuyo,
Hakika umesema kweli.

Lengo la makala yangu ni kueleza kwa nini katika Vita Vya Maji Maji wanahistoria wa mwanzo wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kukwepa majina ya Kiislam?

Ikiwa mimi kufanya hivyo unaona nafanya makosa inakuwaje kwa hawa wanaokwepa kutaja majina ya Waislam wakawataja kwa majina siyo?

Ndipo nikaliweka jina la Bi. Khadija Mkomanile na jina la Abdulrauf Songea Mbano.

Bahati mbaya kama wewe unaumizwa na hizi juhudi zangu za kusahihisha historia hii.
 
Sema historia yetu inawatenga sana wanawake hata Bibi Titi historia ya ukombozi wa Nchi haimuongelei kabsa lkn ni katika wanawake waliokua mstari wa mbele kwenye ukombozi wa taifa letu dhidi ya mkoloni..
Picha kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed na kushoto wa.kwanza ni Bi. Tatu bint Mzee.

Uwanja wa Ndege Dar es Salaam wanamsindika Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO 1955.
 
Mzee
Nashukuru umetuletea kumbukizi jadidi ya vita yaMajimaji ingawa naona wanzuoni wa Islam mmeanza kuiteka na kuibadili kuiita Jihadi ya Majimaji... sijajua lengo mahsusi.

Sasa nakusihi tuletee usuli kuhusu bi Khadija Nkomanile....
 
Mzee
Nashukuru umetuletea kumbukizi jadidi ya vita yaMajimaji ingawa naona wanzuoni wa Islam mmeanza kuiteka na kuibadili kuiita Jihadi ya Majimaji... sijajua lengo mahsusi.

Sasa nakusihi tuletee usuli kuhusu bi Khadija Nkomanile....
Msanii,
Historia ya.Maji Maji ina mengi.

Soma barua ya Nduna Abdulrauf Songea Mbano kwa Sheikh Mataka Hamim Massaninga unaweza ukaelewa.
 
Natamani nikutane na wewe Mzee Said Kuna vitu nataka kujifunza nataka nikuone.
 
Sema historia yetu inawatenga sana wanawake hata Bibi Titi historia ya ukombozi wa Nchi haimuongelei kabsa lkn ni katika wanawake waliokua mstari wa mbele kwenye ukombozi wa taifa letu dhidi ya mkoloni..
Hawa ndio super women,nyie mmewapa wake zenu kwa Sababu ya kuwapikia ugali.Wengine wanajihita Superwoman kisa kagawa vijora shuleni.Siku ya leo ilikuwa kumbukizi ya Hawa wanawake ambao kivuli chao kinaishi.
 
Mzee Mohamed wewe mashujaa wako ni waislamu tu,sijawahi kuona ukiwasifia wakristo waliopigania uhuru.
 
King Kong III,
Historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika imejaa visa na mikasa mingi ya Waislam na sababu ni kuwa wao ndiyo walikuwa wengi kwenye harakati.

Hupendi kusoma historia hii?

Nakufuatilia sana Mkuu Mohamed ,kwenye historia ya uhuru tuliambiwa kwamba Mzee Aikaeli Mbowe(Mkristo) alimchangia pesa Mwalimu nyerere ya kwende UNO na alikuwa mfadhili wa harakati nyingi za kupigania uhuru lakini watu kama hao hauwazungumzii kwasababu ni wakristo ,angekuwa muislam ungemzungumzia kama yule aliyetoa kiwanja cha ccm ofisi ya lumumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…