Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BI. TITI MOHAMED BADO ANAISHI KATIKA SIASA, MAENDELEO NA FIKRA ZA WANAWAKE WA TANZANIA
Kwa kipindi cha majuma mawili kabla ya maadhimisho rasmi ya kumbukumbu ya Bi. Titi Mohamed Ikwiriri nimekuwa nikipokea wageni katika Maktaba yangu wakitaka kunihoji kuhusu maisha ya Bi. Titi Mohamed.
Nikipokea simu kutoka TBC wakiniomba wafike kwangu kwa ajili ya mazungumzo kuhusu Bi. Titi na nikawakaribisha tukafanya mahojiano kwa takriban saa moja.
Jioni yake katika kipindi mashuhuri cha habari Maridhio Bi. Titi akawa hewani akaonekana akiwa kasimama kwenye jukwaa la kujengwa kwa miti pembeni ya Julius Nyerere katika Viwanja Vya Jangwani wakihutubia wananchi.
Hii ilikuwa clip ya "black and white," yaani si picha ya rangi.
Hiii ilikuwa miaka ya katikati 1950 TANU kwa ukubwa wa mahudhurio ya wananchi kwenye mikutano yao uwanja wa Mnazi Mmoja ulikuwa mdogo hautoshi kamwe sasa wamehamia Jangwani.
Bi. Titi anaonekana akiwa bado msichana mdogo wa miaka 30 mwanzoni.
Nakiangalia kipindi nauna hii clip ya Bi. Titi na Mwalimu Nyerere, sauti yangu naisikia inaeleza historia ya Bi. Titi na namtaja pamoja na wenzake, Bi. Tatu bint Mzee, Hawa bint Maftah na Bi. Halima bint Khamisi.
Kipande hiki hakikuzidi dakika mbili hivi na lau kama historia hii naijua vyema nilitamani kama kipindi kizima kingekuwa ni historia ya Bi. Titi Mohamed.
Siku ya pili mchana bila taarifa TBC wakanivamia vijana wakanitaka radhi kwa kuja ghafla wakanieleza kuwa wanataka kurusha kipindi kingine usiku siku ile cha Bi. Titi.
Haya Bismillah...
Huyu ni msichana ananihoji kuhusu Bi.Titi na maisha yake ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Lakini jana tu mimi na TBC tumemzungumza Bi. Titi hofu tayari imeshaniingia kuwa kuna hatari ya mimi kujirudia.
Nachelea sitamtendea haki Bi. Titi wala watazamaji wa kipindi.
Ikanijia fikra.
Huyu ananihoji ni msichana napima umri wake naona Bi Titi alikuwa umri wa huyu binti wakati anaanza harakati za kupigania uhuru.
Huyu binti aliniambia tutafanya mahojiano mafupi lakini naona tunazidi kuzungumza.
Historia ya Bi. Titi ya miaka ya 1950 akihamasisha vikundi vya akina mama vya Saniyyat Hubby, Coronation na Alwatan kuipa nguvu TANU kwa nyimbo na muziki wa taarab.
Hakika huyu bint historia hii ilikuwa imemchukua sana.
Usiku ule Bi. Titi akawa tena hewani.
Siku zilizofuata hali ikawa kama hivi.
Online TV, magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Habari Leo.
Wakitoka hawa wanaingia wale.
Maofisa wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wakanifikia.
Hii ilikuwa timu kubwa ya wataalamu wanatengeneza "documentary," ya Bi. Titi.
Bi. Titi, Bi. Titi, Bi. Titi...
Wote wanataka kusikia historia ya Bi. Titi na wanataka niwape picha za Bi. Titi.
Jana usiku nimewasili Ikwiriri kwa mwaliko wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Mohamed Mchengerwa kushiriki katika tamasha la Bi. Titi.