Biashara au kampuni inapofungwa kimyakimya bila ya wafanyakazi kujua mwelekeo wao

Nkyumu

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2012
Posts
332
Reaction score
104
Ukiwa umeajiriwa na kampuni binafsi ikaja ikatokea mmiliki wa kampuni halipi mishahara inafika mahali hata ofisi halipii jengo ilipo, landlord anafunga ofisi na mamlaka za serikali nazo zinaongezea makufuri yake (Jiji) .

Kisanii mmiliki anafanikisha kuhamisha mali za kampuni ingali kwamba wafanyakazi hawajui muelekeo wao.

Ni ushauri gani au maamuzi yapi wafanye?
 
Hapo inabidi hatua za kisheria zifuatwe hasa sheria zinazomlinda mfanyakazi lakini jambo la kwanza una mkataba na hiyo kampuni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…