Biashara endelevu

JOSEPHAT.P

Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
70
Reaction score
18
Mjasiriamali mwenzangu,yakupasa kufanya biashara kwa manufaa ya leo na kesho! Anza kidogo upate uzoefu kisha ongeza wigo wa mtaji ili kuweza kutumia maliasiri zilizopo kwa ufasaha zaidi kwani utakuwa umeshatambua fursa na changamoto katika sekta yako! Pia kumbuka kuwa ili biashara iweze kuleta faida ni lazima ujue wateja wanataka nini, kwa kiasi gani, wapi na wakati gani.
Vijana tuamke na tuchangamkie fursa, mfano: ukiwa na kuku wa mayai 500 ambao unanunua kwa sh..2500,ukafuga nyumbani, unalisha kwa muda wa miezi 4, halafu mwezi wa tano unaanza kuuza mayai. Hii ni biashara nzuri sana pale itakapochukuliwa uzito!
Pamoja tunaweza na daima pambana kupunguza umaskini wako mwenyewe.
 
Nafurahi sana vijana wanapopeana mawazo katika kukabiriana na kuushinda mzunguko wa umasikini. Mawazo mazuri sana, ila kuku mmoja anatumia wastani wa 10,000/= mpaka atage, mradi wa kuku 500 utahitaji kama +5M. Itakua vema zaidi kama tutaweza kuwaangalia pia vijana wenye uwezo wa chini ya hapo pia
 
Thanks mkuu,nadhani hao kuku mia tano umetoa kama mfano mtu,zaidi ya hapo kijana anapaswa kuangalia uwezo wake kwamba afuge kuku idadi hiyo au la,anze na biashara nyingine
 

Mkuu umetoa angalizo zuri.

Lakini, kuna Msemo wa Wahenga usemao "Umoja ni Nguvu, Utengano ni Udhaifu". Vijana, unaowaongelea, wakiweza kuweka ubinafsi pembeni, wakaungana hili linawezekana. Nimeshuhudia hili kwenye Vikundi vya HISA, pamoja na kuwa ni katika manthari tofauti. Nimeona mwenyewe jinsi nguvu za Kikundi zinavyoweza kubadili maisha ya Wanachama wake hasa kupitia IGA's za Wanachama hao.
 
Nakubaliana nawe katika mtazamo huu, kupata mtaji kwa njia ya kibati/vicoba n.k, kumeonyesha matokeo chanya na labda ndio njia tunayojisimamia wenyewe "masikini" iliyo na mafanikio. Rasilimali alizonazo masikini wa Tanzania zikitazamwa kwa upande mwengine zinaweza ku-mpa utajiri, kwa hilo watoto wa masikini wenye elimu wakituelimisha ndugu zao tatutoka. Mfano kuna jamaa wanajiita HIMA niliwaona kanda ya kusini wakifundisha matumizi bora ya ardhi na kilimo cha mchanganyiko na miti vitu vilivyo watoa sana ndugu zetu wa huko.
 
Ni kweli kabisa, kwani huo nilitoa kama mfano wa biashara ambayo mtu anaweza kuanza nayo lakini kuanza kidogo ni kuzuri sana, mfano hivi vijana wanajua kuwa katika kila kata wanazoishi kuna uwezekano wa kufungua Community Based Organizations(CBO)? Hivyo bhasi wakianza kama CBO wakasajiri kwani ni kama elfu90 kusajiri then wakapata mkopo ambao hauna riba. Changamoto nyingine kwa sisi vijana ni kwamba hatufuatilii taarifa za opportunity katika kujiajiri.
Tuongeze juhudi kwa kila kitu cha maendeleo! Hivi jamani mmeshawahi kujiuliza ni kwanini Wahindi wanafanya biashara mahali wanapoishi? yaani chini biashara juu makazi. I KNOW WE CAN
 
Kwa wale wajasiriamali ambao hatuna mtaji wa kutosha na tunataka kukopa fedha ili kuanzisha biashara, ni jambo jema sana lakini mara upatapo huo mkopo ni vema ukatumia SWEAT EQUITY RATIO.......yaani jasho lako liweze kuzalisha kipato na kuongeza mtaji wako na sio kuwa boss kupita kiasi.
Tujitume na tuache kulalamika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…