Biashara gani naweza kufanya kwa mtaji wa TZS 500,000/=?

Biashara gani naweza kufanya kwa mtaji wa TZS 500,000/=?

lazima ukae

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2013
Posts
791
Reaction score
414
Habari zenu wapendwa

Naomba mnipe msaada wa mawazo kuhusu biashara ambayo naweza kufanya kwa mtaji wa Tshs 500,000

Hata kama ni yakusafiri sio mbaya
 
Ukiwa boder kama tunduma, kasumuru au boder yoyote unaweza kufanya biashara ya kubariki fedha. Ni biashara nzur kwakuwa inatoa majibu ya papo kwa hapo cha msingi zifahamu changamoto za biashara hii na jinsi ya kukabiliana nazo kabla hujajitosa.
 
Upo wapi!! Kama upo dsm kuna biashara ya maziwa toka mkuranga pwani au toka kibaha kwa wafugaji (pastoralist) inalipa watakuuzia lita 900/= 1000/= 1200/= kuna uwezekano wa kupata lita 100, 150 mpaka lita 200 hayajachakachuliwa toka kwa ng'ombe wa kienyeji ukifikisha dar es salaam unauza kwa jumla cafe au hotel au kwa mama ntilie na kusambaza mtaani kila siku pato lako kwa siku litakuwa 40,000/= hapo umetoa garama zote nauli na uchovu
 
Mbona hujasema dar atayauza kwa sh ngapi
 
Dar es salam maziwa kwa jumla yanauzwa 1500/=, 1600/= kwa lita mkuranga, rufiji kibaha wasukuma wanauza 800/=, 900/= mpaka 1000/= kwa lita ila hupatikana vijijini ndani ndani
 
Back
Top Bottom