Biashara gani ya kufanya kisiwani Mafia

Biashara gani ya kufanya kisiwani Mafia

Joined
Aug 4, 2014
Posts
21
Reaction score
7
Wakuu, kwa wale wanao kijua vizuri kisiwa cha Mafia, naomba msaada ni biashara gani naweza kupeleka uko na ikatoka haraka. naomba mnisaidie, mdogo wenu. Natanguliza shukrani kwa wale watakao nipa mchango wao.
 
habari yako mdogo wangu kwanza wewe ushawahi fika mafia, kwa upande wangu mimi nishapuyanga visiwa vyote hapo kuanzua hapo kilindoni, hadi visiwa vya nje vya mafia kama chole, juani, na kibondo....mimi hapo nilikuwa nafanya biashara ya uvuvi...ila kwa wewe mafia kuna fursa kuu mbili.

(1) biashara ya mafuta Petrol na diesel...Mafia kuna sheli mbili tu bado haikiji watumiaji wa vyombo vya baharini na bodaboda na magari (2) fungua gesti ya kisasa ..Mafia inakuwa ki utaliiii watu na wageni wanakuja tembea huko..kwa hiyo gesti zinalipa (3) bidhaa kupeleka kama Ngano, unga wa Sembe mafuta ya kupikia n.k ila hiyo ina changamoto yake katika usafirishaji.sasa wewe ulikuwa na idea ipi hapo.
 
Ahsate mkuu kwa ushauri wako, ila kuhusu biashara ya mafuta, guest hiyo siiwezi mtaji wake mkubwa sana. mimi nina kamtaji kadogo sana tu labda biashara ya ngano, unga na mafuta. naomba kujua change moto za usafiri ni zipi? mkuu kamtaii kangu kadogo sana shs 7milion tu mkuu
 
Kabla hujafanya lolote nakushauri nenda Mafia ukajionee, ujuane na wenyeji wafanya biashara wa pale ili uelewe hali halisi.

Usichukuwe ushauri kwa mtu ambae hafanyi biashara. Nenda.
 
ulishawahi fika mafia unge jaribu kwenda ukafanye research huko we mwenyewe, changamoto kubwa ta usafiri ni kwamba unapo nunua bidhaa unaenda kuzipakua kwenye majahazi ....kisiju mzigo unakwenda kwa majahazi, wewe unakwenda kwa boti la kawaida.kuna wakati mwingine jahazi linazama na mali yote na majahazi hawana bima...mali ikizama imekula kwako, kwa hiyo hali kama hiyo ni bahati mbaya ikitokea...
 
Kabla hujafanya lolote nakushauri nenda Mafia ukajionee, ujuane na wenyeji wafanya biashara wa pale ili uelewe hali halisi.

Usichukuwe ushauri kwa mtu ambae hafanyi biashara. Nenda.

mimi nampa ushauri kwa sababu nishakaa kwenye kisiwa hicho nakijua in n out.....ila bado haimanishi yeye aende tu kuanza biashara kama unavyosema....aende mwenyewe akajioneeee huko akakutane na wakojani huko akaseme nao..
 
Kabla hujafanya lolote nakushauri nenda Mafia ukajionee, ujuane na wenyeji wafanya biashara wa pale ili uelewe hali halisi.

Usichukuwe ushauri kwa mtu ambae hafanyi biashara. Nenda.

Daah..umemshauri vizuri sana..
 
Nawashukuruni wote kwa mchango wenu, nitaufanyia kazi, nitaenda kufanya utafiti kabla ya kuanza biashara na baadae nitawarudia kuwapa ripoti. mbarikiwe
 
Ahsate mkuu kwa ushauri wako, ila kuhusu biashara ya mafuta, guest hiyo siiwezi mtaji wake mkubwa sana. mimi nina kamtaji kadogo sana tu labda biashara ya ngano, unga na mafuta. naomba kujua change moto za usafiri ni zipi? mkuu kamtaii kangu kadogo sana shs 7milion tu mkuu

hivyo pesa nyingi na inatosha kufanya biashara kwa hapo mafia nenda kaangalie zipo fursa nyingi tu
 
Nawashukuruni wote kwa mchango wenu, nitaufanyia kazi, nitaenda kufanya utafiti kabla ya kuanza biashara na baadae nitawarudia kuwapa ripoti. mbarikiwe

ukienda huko wasiliana na huyo jamaa ni mfanyabiashara wa siku nyingi huko ana duka kwabwa anauza ngano, mahindi, mafuta ya kpikia, sukari..etc anaagiza mzgo toka dar anaitwa amiri...namba yake hiyo 0787621232 anairwa amiri..
 
habari yako mdogo wangu kwanza wewe ushawahi fika mafia, kwa upande wangu mimi nishapuyanga visiwa vyote hapo kuanzua hapo kilindoni, hadi visiwa vya nje vya mafia kama chole, juani, na kibondo....mimi hapo nilikuwa nafanya biashara ya uvuvi...ila kwa wewe mafia kuna fursa kuu mbili.

(1) biashara ya mafuta Petrol na diesel...Mafia kuna sheli mbili tu bado haikiji watumiaji wa vyombo vya baharini na bodaboda na magari (2) fungua gesti ya kisasa ..Mafia inakuwa ki utaliiii watu na wageni wanakuja tembea huko..kwa hiyo gesti zinalipa (3) bidhaa kupeleka kama Ngano, unga wa Sembe mafuta ya kupikia n.k ila hiyo ina changamoto yake katika usafirishaji.sasa wewe ulikuwa na idea ipi hapo.
Nafikiri hicho kisiwa kingine sio kibondo kinaitwa Jibondo Mkuu. Nmefika huko watu kisiwa kizima wanaishi kama familia moja. Kibondo ipo Kigoma.
 
ukienda huko wasiliana na huyo jamaa ni mfanyabiashara wa siku nyingi huko ana duka kwabwa anauza ngano, mahindi, mafuta ya kpikia, sukari..etc anaagiza mzgo toka dar anaitwa amiri...namba yake hiyo 0787621232 anairwa amiri..
Pia kuna ardhi nzuri sana yenye malisho mazuri. So unaweza fuga ng'ombe kule kama utakuwa na njia ya kusafirisha kwenda bara. Niliwaona wasukuma wengi kule wanafuga ng'ombe
 
Nafikiri hicho kisiwa kingine sio kibondo kinaitwa Jibondo Mkuu. Nmefika huko watu kisiwa kizima wanaishi kama familia moja. Kibondo ipo Kigoma.
Jibondo ndiyo, nmekaa pale

Ova
 
Back
Top Bottom