Niko naangalia Aljazeera kuna documentary wanaonesha kuhusu utafiti wao juu ya biashara haramu ya pembe za ndovu na faru. Wameanzia Afrika Kusini mpaka China na Vietnam ambako ndiko kuna masoko ya bidhaa husika. Ukweli inasikitisha sana jinsi maliasili ya Afrika inavyokwisha tkwa kasi huku nchi zetu zikikumbatia watu hawa na biashara yenyewe.
Documentary inaonesha jinsi Waziri wa Usalama nchini Afrika Kusini ambaye ana jukumu la kusimamia na kuendesha kampeni za usalama, akiwa mtu wa karibu sana kwa wachina wanaofanya biashara ya kununua na kuuza pembe hizi huko China. Pia wanaonesha jinsi vyombo vya usalama vinavyoweza kuhongwa na kushindwa kusimamia suala hili. Na wachina wanaohusika wanasema Afrika kila kitu ni pesa tu wakimaanisha wanafanikisha haya kupitia mfumo wa rushwa uliopo. Kibaya zaidi ni wachina hawa kukiri kuwa ziara za viongozi wao, mfano Rais wa China, nchini Afrika Kusini zinafanikisha kuuzwa kwa meno haya maana diplomats na members wa delegation wananunua kwa wingi na kusafirisha kwenda China (nahisi ni kwa sababu hawakaguliwi popote, na hata kama wanakaguliwa, mfumo wa rushwa uliopo siyo rahisi kukamatwa).
Huko China na Vietnam inaonesha mpaka maafisa wa serikali wanashiriki kwa karibu kufanikisha biashara hii haramu kupitia mtandao huu. Its really shocking, nadhani miaka michache tu imebaki tutakuwa hatuna tena wanyama hawa. Nimejiuliza, wakimaliza tembo na faru watahamia kwa wanyama gani? Sijaweza kupata jibu kichwani mwangu.
Unaweza kuona documentary nzima kupitia documentary hii