Biashara haramu zenye kufadhiliwa na Mamlaka za Serikali

Biashara haramu zenye kufadhiliwa na Mamlaka za Serikali

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana sasa hii nikiwa mjini kurejea maskani tokea hija - kanda pendwa. Safarini vituko ni vingi tokea kwenye operation kukusanya 30,000/= @ gari hadi biashara haramu chini ya mamlaka za serikali alimradi kazi inaendelea.

Operation kusanya pesa nilileta uzi kamili:


Leo hapa, nisiache kuangazia biashara haramu zinazofadhiliwa na Mamlaka huku wakiwawekea ugumu wa utendaji ulio wazi wale ambao haswa ndiyo walio walipa kodi:

1. Biashara ya wizi wa mafuta kwenye malori.

Waziwazi mabarabarani kuna biashara rasmi za wizi wa mafuta kutoka na kwenda kwenye magari zinazoendelea bila kificho wala woga wowote, almaarufu kupiga videbe.

Biashara haramu hii wana hisa wake wakuu ni polisi. Kwa mwezi rasmi huwazungukia mawakala wao wa wizi wakikusanya magawio yao kwa michango yao muhimu ya kufanikisha kufanyika kwa biashara hii pasipokuwa na usumbufu.

1. Biashara ya kusafirisha abiria kwa magari madogo (mengi yakiwamo probox, nk) almaarufu - mchomoko, bila leseni husika.

Magari haya wengi wa wamiliki wake ni polisi hasa wale wa usalama barabarani. Magari haya, hayana leseni husika tokea LATRA.

Kwa kutambua hizi ni mali za wakubwa LATRA wameuchuna kama vile hawaoni, hivyo kazi inaendelea!

Maswali ya msingi ya kujiuliza ni kuwa:

1. Mwenye lori anapoibiwa mafuta yake kwa ufadhili unaotolewa na polisi anayelipwa kwa kodi ili alinde mali za akiwamo mwenye lori ambaye pia ni mlipa kodi, pana uhalali gani wa polisi kuendelea kuwapo?

2. Magari yasiyokuwa na leseni ya kubeba abiria yanapovamia biashara ya soko dhidi ya wenye leseni na wanaolipa kodi huku wakifadhiliwa na waliopaswa kutoa usimamizi yaani polisi na LATRA, pana uhalali gani wa mamlaka hizi kuendelea kuwapo huku zikiendelea kuwadai kodi wale ambao wao wanakandamizwa na hao hao wadai kodi?

Ajabu na kweli ya fyongo haya yanatokea ndani ya nchi hii hii ambapo TAKUKURU nao wapo na wanaagalia tu kama walivyo wapenzi watazamaji wengine wowote.
 
Hi nchi ngumu Sana wasimamiz wa Sheria ndo wavunjifu wakubwa

Tembeeni kuona. Huko pembezoni mamlaka ni miungu watu. Kwa hakika ingekuwa huku pangechimbika.

Biashara mbili hizi zimeshamiri mno kwa hisani ya Polisi na LATRA.

What a shame?
 
Back
Top Bottom