Biashara hii inakwendaje na itapokelewaje?!

visa gold

Member
Joined
Sep 12, 2013
Posts
41
Reaction score
4
FHabari za ninyi wanaJF,

Nimekaa nikawaza kutokana na ukweli kuwa watanzania wanapenda sana utamaduni wao mnahisi itapokelewaje biashara hii ya kuandaa kadi zilizo katika lugha ya kiswahili?! Yaani muundo ule ule lakini maneno ndo ya kiswahili chetu?! Mnadhani itafaa?!

Nahitaji maoni yenu hapo tafadhali. Naombeni msipite bila kutoa wazo lako. Naomben sana
 
Itakuwa vizuri sana ingawa watanzania tumegubikwa na ulibumbukeni wa kizungu ila tunaojua na kukithamini kiswahili chetu tutanunua! Andaa tu mtu wangu.
 
Asante sana kwa ushauri unaonipa moyo ntajaribu Mungu anisaidie navyojua ilimradi kiwe kizuri wananch hawana shida nayo. Nashkuru sana baba ziro
 
Kaka kwanza naomba nikupongeze kwa ubunifu wa wazo hilo, mimi naamini ukiwa unazibuni vizuri na kweli zinapendeza machoni na maneno mazur zinauzika tu hata mimi nisiyependaga kadi nitanunua bana!!
 
Good Idea,
Jaribu kutafuta washauri wa namna ya utohoaji wa amaneni ya kiswahili ili ivutie.Hii ni fani pia.
Unaweza wewe ukawa na wazo lakini ukawa namtu pembeni ni mjuzi wa maneno ya kuvutia.Hasa watunzi wa mashairi ni mahodari sana wa kucheza na maneno.Mcheki Mrisho Mpoto akupe Ideas
 
tungepata km ninyi laki sijui tungekua wapi kimaendeleo
 
wazo zuri sana!
haya kazikwako weka katika vitendo!!
kila la kheri
 

Hebu jaribu mkuu, naona kuna potential ya kibiashara kwenye wazo lako, na unaweza kuuza hadi ukashangaa. Kila siku watu wanataka products mpya sokoni. Hope utauza sana.
 
Nashkuru sana wadau kwa kunipa moyo. Nilidhani ni wazo la kitoto lakin kwa moyo huu mlionipa itabidi nichangamkie fursa nimepanga kuanza na soko la wanafunzi nikisambaza angalau stationary za mavyuoni niangalie response zake kwanza.

Nahitaji msaada zaidi wadau... taarifa zaidi ya nilipofikia ntawataarifu hapa hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…