Maana yake una ukwasi mwingi kupita kiasi na hiyo biashara huijui vizuri na yumukini wateja wako huwajui vizuri vionjo vyao.
Mara nyingi hali hiyo huwapata sana wastaafu baada ya kupata malipo ya mkupuo na kujiingiza moja kwa moja kwenye biashara kwa kufuata mkumbo maarufu wa kujaza bidhaa hadi nje ya duka.
Kwa bidhaa zenye ukomo wa matumizi huishia kuteketezwa, ambayo kimsingi ni kuteketeza mtaji na kuwa mlango wa kutokea.... Kufunga biashara!.