kitalembwa
JF-Expert Member
- Jul 12, 2014
- 3,607
- 9,430
Naam tunaimalizia August,,,
Back then nikiwa chuo(sikufanikiwa kupata boom) Kuna michongo nilikuwa nafanya ili kidume ni-survive mjini,,, ! Hii ilipelekea performance kushuka Sana, mda mwingine hadi nilikuwa namlipa mtu ananifanyia assignment, n.k!!
Moja ya mchongo niliokua nafanya Ni kununua mchele na maharage(naagiza mbeya) alafu nazunguka madukan kuuza,pamoja na mama ntilie! Sikua na mtaji mkubwa Sana, nilikua naagiza kilo 800-1000 za mchele, pia kgs 600-700 za maharage! Nilichokuwa nafanya kwa mtaji huu mdogo Ni kwamba nawauzia madukan huku nikiwaachia nao faida kdg mzigo uishe niagize mwingine,,,mfano kipindi hicho (2012-2016) nilikuwa nanunua mchele super kwa 1300, mm nauza 1700 ili muuza duka auze 1900/2000, maharage pia niliuza kwa style hio ! Mzigo unaisha haraka unaagiza mwingine,,, !! Hapa nilikuwa najikimu vyema kuanzia Kodi ya geto, kuvaa, gharama za chuo n.k!!!
Nilikuwa nikimaliza mzigo natuma hela natumiwa mzigo,, Sasa bwana Kuna siku nikatuma hela, jamaa kimya, siku ya nne kimya, wiki kimya,, ! Jamaa akapita na ile hela, nilichanganyikiwa, nakumbuka nilishinda ndani Kama wiki kwa uchungu, alieniunganisha nae nikaenda offcn kwake mbez kipindi hicho, nae namkuta ana majanga zaidi yangu , kakimbia na hela ya mzigo fuso nzima, ! Tulimfatilia bila mafanikio, tukaja kuambiwa alitapeli watu wengi na mbeya alihama kabisa, Kuna wakulima wanamdai pia! Niliishi kwa shida kiasi kwamba mpaka pc yangu niliiuza!
Baada ya kumaliza chuo, wakati nahangaika kupata kazi, home walijichanga na sister akakopa job kwao nikapewa Kama Kama 5m nikafungua duka genge,,,, mwanzo Mambo yakaenda fresh kabisa,,, !! Kuna jamaa namjua, aliomba nimdhamini apewe bajaji,,, nikajichanganya, mshezi baada ya Kama two months, akampa mwanafunzi mimba, akakimbia na ile bajaji,,, ! Kesi ikawa kwangu, mzee akawa mbogo, tukaandikishana police kila mwisho wa mwezi nikawa nampa kiasi kadhaa, bishara ikayumba, sister nae akafiwa na mumewe,,, kipato kikapungua, kila saa usumbufu anataka hela , hatimae duka nikachemka nikafunga,,,,
Kama bahati, Kuna mdada humu nilikuwa nawasiliana nae kitambo Sana enzi Niko chuo, Ni mtu mzima flani (nilishaleta story yake humu, miaka 6 ya Jf) ndio akanipa mchongo kupitia mume wake nikaajiriwa rasmi, ndo ninapofanya kazi mpaka leo,,, !!
Biashara sikukata tamaa japo nilipata kazi, bado Niko nafanya mishe zangu flani flani nje na kazi yangu rasmi , maisha yanasonga namshukuru Mungu kwa Hilo! Nimejikuta nakumbuka nilikotoka, na roho ya kutokukata tamaa, biashara zinahitaji Sana akili, nguvu, uaminifu n.k hasa kwa mtu ambaye muda wako haukutoshi kusimamia shughuli zako nyinginezo, ukijichanganya unafunga biashara, nilichogundua pia ukiwa muoga muoga biashara itakushinda, lazima uwe risk-taker!!!!
Happy Sunday !!