Tatizo la ugumu wa biashara Tanzania linasababishwa na mambo mawili makuu, kwa wale wanaonunua biashara nnje kikwazo kikubwa ni Dola,Nitatoa mfano:Ukinunua bidhaa nje kwa dola 100USD,ambayo nisawa na 150,000Tsh. tujaalie ni mwezi wa may, 2011,uliuza bidhaa hiyo kwa 180,000.utaona umeingiza faida 30,000, sio mbaya.lakini mwezi wa oct, 2011 unataka ukanunue tena hile bidha ili uje uuze tena ukienda kununu dola utaikuta imepanda kutoka 150,000 hadi kufikia 180,000 kuinunua wewe ,inamaana ile fada amboyo iliipata imekufa na umerudisha gharama tu kama hujala hasara. sasa unakua unafanya kazi bure au kwa hasara, kwa mpango huu lazima biashara iwe ngumu.
kwa wale wenye mitaji mikubwa ndio huendelea kwa sababu wao hununua vitu bei ya chini pengine kwa order ya kontena moja au mawili sasa lile tatizo la dola kupanda wao huwaathiri gidogo sana.
Ama kwa wafanya biashara ya ndani ni mitaji huwa ndio tatizo,kwa mfano: mahidi yanapokua kwa wingi hua yanashuka bei,sasa faida hua ndogo sana kwani ushindani huamkubwa,na mahindi yakiisha msimu yanakua ghali sana kiasi ambacho wafanya biashara wadogo wanashindwa kuyanunua na hata akiyanunua kwa kutumia ule mtaji mdogo basi atashindwa transport, sasa hapa ndio biashara hua ngumu, lakini kwa wenye mitaji hupeta kwa kua wao hununua kwawingi hule muda wa msimu na msimu ukimalizika yeye ndio anauza mali yake.
Kwa kujibu kwakutumia neno moja linalo yaunganisha maelezo yangu nikua MTAJI NDIO TATIZO katika biashara za kibongo.
mambo mengine madogo madogo ndio hayo ya umeme,kuenea kwa bidhaa feki pia kunachangia biashara kua ngumu,udhibiti wa bei serekalini pia huchangia,rushua pia nitatizo kwasababu mwenye makontena matano ya atatoa rushua bandarini alipe milioni tano ambayo sisawa na ushuru wa kontena moja,lakini mwenye kontena moja atalipa hio hio milioni tano,sasa yule mwenye kontena tano atakushinda uwanjani,wewe utauza bidhaa kwa 1000 na yeye bidhaa hio hio atauza 300 sasa kwanini biashara isiwe ngumu? na yako mambo mengi mengine pia ufahamu wa wateja mtu atahiari anunue feki kwa rahisi kuliko kununua original kwa kwa bei kubwa kidogo.