Biashara inahitaji huduma nzuri sana au kujitangaza sana

Mapensho star

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
3,052
Reaction score
4,104
habari za siku natumaini ni wazima
kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu
kwanza niseme ni mara chache sana kukuta kampuni au biashara ina toa huduma nzuri sana na kujitangaza sana vyote kwa pamoja

utakuta kampuni inajitangaza sana lakini huduma ni za kawaida sio mbaya ila kuna mapungufu na mfanyabiashara unakuta anafanikiwa kuliteka soko

vile vile utakuta mtu mwingine anatumia nguvu nyingi kuweka huduma nzuri sana lakini kujitangaza sio sana na pia yeye anafanikiwa kuliteka soko

lengo la kuanzisha uzi nikutaka kujua biashara inahitaji ratio ya asilimia ngapi kati ya kujitangaza sana na kuwa na huduma nzuri sana
wataalamu na wenye uzoefu wa biashara mtusaidie
 
Biashara ni matangazo huduma inakuja baada ya kujitangaza ukitaka utoe huduma nzuri ndo biashara ijitangaze utachelwelewa sana mkuu

Jitangaze kwanza ili watu waijue biashara yapo ni gharama sana
 
Mambo haya yana nguvu kubwa sana "Karibu, tabasamu, asante ". Ukisindikiza na usafi pia mpangilio mzuri wa lugha na bidhaa zako wateja watajaa kwako bila hata ya kutumia nguvu ya kutangaza biashara yako itajitangaza yenyewe. Amini nawaambia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…