Fanya biashara ya kukopesha pesa (vikoba). Kopesha elfu 50 tu kwa kila mfanyabiashara mdogo mdogo na riba ni 10,000 kwa 15,000 kwa wasumbufu, na wale wasio sumbua ni 10,000 kwa 13,000.
Mwanzo ni mgumu sana maana itakuchukua muda ili kijulikana na watu ila wateja wakishajua ww ni mkopeshaji, ww ni kupiga pesa tu.
Ila kabla ya yote nenda TRA kwanza kaulize kinahitaji nn na nn ili ufanye biashara hyo.
Pia unatakiwa uwe na mbinu ili uweze kudai pesa yako na sio kutumia maguvu kama unanyanyua vyuma, hivyo inatakiwa uandike mkataba mzuri ili uweze kumpana mkopaji.