Biashara kiganjani. Hivi ndivyo unavyoweza kunasa wateja kwa kutumia internet na kujiingizia kipato

Biashara kiganjani. Hivi ndivyo unavyoweza kunasa wateja kwa kutumia internet na kujiingizia kipato

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
N:B: Lazima uwe na ujuzi au maarifa ya kutatua shida, sio kuminya tu simu.

Tafuta ujuzi au maarifa ya kumtatulia mtu shida kwa uhakika na uaminifu. mfano mimi hii ni kazi part time, najihusisha na mini logistics, niliwahi kuandika humu >> link <<

Tengeneza page yako ukionyesha ukamilifu wako kwenye hio idara, mawasiliano, sura yako, n.k. ili mteja anapotaka kukuchunguza ashawishike you are the right person for the job.

Anza kufuatilia page zenye watu wanaotafuta hizo solution.

Anza kusoma comment, zinase zile za watu walio serious kutafuta solution

Wasiliana nao kwa inbox au simu, usiwe na tamaa, kila kitu kina mwanzo hata ukianza na mteja moja kwa wiki.

Unapopewa nafasi onyesha uwezo, ukipewa kazi fanya kweli.

utendaji wako wa kazi taratibu utaanza kukupa jina nao watakuwa wanakutafutia wateja nje ya wale unaowatafuta wewe, brand inakuwa kubwa.

Mafanikio hayaji kwa muda mfupi, inakubidi uwe mvumilivu na consistency deal na sehemu moja at least kwa mwaka mzima, mafanikio yasikutoe nje ya reli.
 
Back
Top Bottom