Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,422
Swali rahisi sana; kama mteja anaweza kununua kwa mtu yeyote, kwa nini aje kununua kwako? Unaweza kujibu swali hili? Kama huwezi upo kwneye hatari. Ila usijali, nipo hapa ili tuweze kusaidiana ili uweze kufikia mafanikio kwenye biashara yako.Kama mteja anaweza kununua kw amtu yeyote na hana sababu nyingine yoyote ya kununua kwako basi huna mteja.
Ndio huna mteja na biashara yako itakuwa ngumu sana. Hakuna ubishi kwamba biashara unayofanya kila mtu anaweza kuifanya na kila mtu anaifanya. Kama unauza nyama kati kati ya mabucha mengine matano ni kitu gani kitamfanya mteja aache kwenda kwingine na aje kwenye bucha lako?
SOMA; Huu Ndio Uwekezaji Bora Zaidi Unaoweza Kuufanya.
Kitu kikubwa kinachoweza kumfanya mteja aache kununua kwa wengine na aje kununua kwako ni pale anapojisikia na yeye ni sehemu ya biashara yako. Hajioni kama mteja tu anayekuja kununua na kuondoka, bali anajiona sehemu muhimu kwenye biashara hiyo. Mteja ataweza kujiona hivi kama wewe utamtengenezea mazingira ya yeye kujisikia hivyo.
Wewe unaweza kufanya hivyo kwa kujua matatizo ya mteja wako na jinsi gani biashara yako inayatatua na pia kw akuwa mshauri mzuri kwa mteja wako kulingana na kile anachotaka kufanya na kinachohusisha biashara yako.Mteja hataka kuona kwamba wewe unafikiria kupata faida tu kwake ila anataka aone kwamba wewe ni sehemu ya marafiki zake, wewe ni sehemu ya washauri wake na kama atakuwa na shida anajua mtu wa kwanza kumsaidia ni wewe.
SOMA; Kazi Kama Bidhaa…Mfanye mteja kujisikia kuwa sehemu ya biashara yako na ataacha kununua kwa wengine na kuja kununua kwako tu.Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa.
Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.