Biashara Leo: Mteja hajui anachotaka, Ila anajua kitu hiki muhimu sana

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,915
Reaction score
3,422
Kama unataka kukuza biashara yako na ifikie viwango vya juu sana basi usitegemee sana maoni ya wateja, hasa kuhusu ni nini wanataka.

Ukiondoa biashara za uchuuzi ambazo mtu anakwenda dukani moja kwa moja kununua sukari, biashara nyingi mteja hajui anachotaka. Ndio hajui ni kitu gani hasa anachokitaka, ila akikipata atafurahia sana.

Sasa hili ndio lengo lako kubwa kama mjasiriamali au mfanya biashara, kujua ni nini mteja anataka, ambacho hata yeye mwenyewe hajui, na kumpatia halafu akaridhika sana.

Mteja hajui ni kitu gani anachotaka ila mteja ana matatizo. Na kama akipata kitu cha kumuondolea matatizo yake, atafurahi sana na atakuwa tayari kulipa ili aondokane na tatizo.

Wakati tulipokuwa tunatumia kanda za muziki hakuna mtu aliwahi kusema kwamba anahitaji cd, ila cd zilivyokuja na zikawa bora kuliko kanda za kawaida kila mtu alizifurahia.

Kabla haijaja facebook, au twitter, au whatsapp au instagram, hatukuwahi kusikia watu wakilalamika kwamba kwa nini hakuna facebook au instagram. Lakini watu walikuwa na kiu ya kuwasiliana na wenzao walioko sehemu mbalimbali kwa haraka na kwa bei nafuu. Watu walikuwa na tatizo la kuweza kutumia nyimbo, picha na vitu vingine. Zilipokuja huduma hizi za kurahisisha mawasiliano, kila mtu amekuwa tayari kuwa mteja.

Sasa umejifunza nini katika haya yote?

Jua watu wana matatizo gani, njoo na suluhisho la matatizo yao na kwa gharama watakazomudu halafu buuuum una biashara kubwa na itakayokuletea mafanikio.
Mteja hajui anachotaka ila anatatizo ambalo anataka litatuliwe. Jua tatizo hilo na tayari una biashara.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa.

Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.
 
Wewe jamaa haya unayoongea kila siku ungekuwa unayaishi ungekuwa millionaire tayari. Hila km kawa wabongo kwa porojo atujambo.
 
Mteja Hajui Anachotaka, Ila Anajua Kitu Hiki Muhimu Sana. Kwa mfano? acha porojo weka mifano.

 
Wewe jamaa haya unayoongea kila siku ungekuwa unayaishi ungekuwa millionaire tayari. Hila km kawa wabongo kwa porojo atujambo.

Umilionea hauji haraka mkuu, kama bado una ndoto hizo umepotoka.
Mpaka kufikia mwaka 2029 nitakuwa bilionea(USD), unaweza kuhesabu kuanzia sasa.
Karibu.
 
achana na hivyo vilivyopita hebu tupe wazo lako wewe jipya

Watu wana matatizo makubwa ya usafiri, njoo na njia bora ya usafiri na unalo soko.
Watu wana mataizo ya nishati, njoo na njia mbadala ya kupata nishati na una soko la kutosha.
Watu wana matatizo ya mitaji ya biashara njoo na njia bora ya kuwawezesha watu kwenye biashara na una soko la kutosha.
Matatizo ni mengi, angalia hata yale yanayokusumbua tu wewe na wanaokuzunguka, leta suluhisho na watu watakuwa tayari kufanya biashara na wewe.
 
vitu vya msingi hivi wabongo wanavipuuzia. mbona habari za siasa mkiwekewa tu thread hamuulizi mnaanza kuchangia? Ndio maana mnakuwa na jealous na wakenya wenzenu wafuatiliaji na watekelezaji nyinyi wabongo waulizaji, wakosoaji na wapuuzaji. Watawaburuzeni tu EAC mpaka mkome mbadilike.
Kuna mtu anafanya tips za ujasiriamali kama hizi anaitwa Dave Crenshaw yupo youtube tips zake anaziita "chaos vs entrepreneurs" na pia anafundisha kupitia Online video tutorials & training | lynda.com namfuatilia pia kama huyu mbongo mwenzangu. Nyinyi subirini awaoneshe mafanikio yake. No wonder mnachukia mkiambiwa mjiajiri na mtu aliyeko kwenye ajira.
 

Tuna safari ndefu sana kama watanzania kuweza kuondoka hapa tulipo.
 
Makirita Amani achana na hizi nguvu hasi huwa zipo tu, we endelea kupambana na kusaidia wengine kimawazo. Hivi vitu kuna watu hawajavizoea kabisa na wengine vimewazidi akili kwa hiyo usishangae.
 
Last edited by a moderator:
Wewe jamaa haya unayoongea kila siku ungekuwa unayaishi ungekuwa millionaire tayari. Hila km kawa wabongo kwa porojo atujambo.

Haya ndio matatizo ya watanganyika, pole sana
 
Kaka Makirita, asante sana binafsi bado sijaanza biashara, ila nakaribia kuanza soon maana nimepata pa kuanzia kama utakumbuka niliwahi kukuomba ushauri juu ya kilimo huko Pugu nina kiwanja huko. Umenifunza mengi naamni haya nitayafanyia kazi muda si mrefu nitakapoanza biashara yangu.

Pia nategemea kulima mpunga na wadau flani wa humu ndani mnamo mwishoni mwa mwaka huu tutaanza michakato, hivyo bado nahitaji mchango wako zaidi. Barikiwa sana.
 
Makirita Amani achana na hizi nguvu hasi huwa zipo tu, we endelea kupambana na kusaidia wengine kimawazo. Hivi vitu kuna watu hawajavizoea kabisa na wengine vimewazidi akili kwa hiyo usishangae.

Asante sana mkuu, hili nalielewa sana kwamba kuna watu hasi sana. Na mara nyingi unakuta hawajiamini wao wenyewe na hivyo hawaamini chochote wanachoambiwa.
Huwa sijibu coment hasi, ila mara moja moja huwa napenda kuwafanya hata wafikiri hasi wafikiri zaidi ya hapo, kuwanyima sababu ya kuwa hasi.
Ila comment kama hizi hazinidhuru hata kidogo.
 
Last edited by a moderator:

Asante sana mkuu na karibu wakati wowote.
TUPO PAMOJA.
 
Nilipoona andiko hili nilitarajia wachangiaji wengi waulize au kuomba miongozo ya namna ya kuboresha au kuanzisha biashara zao kwa kutumia points hizo hapo juu BADALA yake sasa duuh! Kweli miafrika ndivyo tulivo !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…