Biashara na Iran

BORGIAS

Senior Member
Joined
Jun 3, 2012
Posts
134
Reaction score
57
Hivi kama mtu una channel ya kuleta wawekezaji toka Iran kuna zengwe lolote serikalini?

Jamaa ninadeal nao na naona wako straight kuliko waarabu wa Saudia, UAE na kwingine

Nishafanya nao biashara Zambia na Mozambique hawa wa Iran lakini naona bongo kuna zengwe left and right

Je mnanishaurije?

Jamaa pesa wanazo na hawana matatizo ya kuinvest kwenye sekta zote.
 
Wiki hii, TD bank ya Canada imefunga baadhi ya akaunti za wateja wake ambao kwa asili ni raia wa Irani na wamekuwa ama wakituma pesa au kupokea pesa toka Irani. Sababu zikiwa ni vikwazo ambavyo nchi ya Irani imewekewa.

Pia, Rais wa Tanzania amalimwa barua na mbunge toka nchi za Magharibi kwa ajili ya bendera za Tanzania kupeperushwa na meli za Iran. Hivi sasa serikali yetu inapambana na hilo jambo kuona kama itatotoa mjibu ya kuwaridhisha wakubwa hawa.

Unganisha haya mawili pamoja na ushauri mwingine utakao pewa na wanaJF wengine, alafu fanya maamuzi yako.
 
Mkuu kama wewe ni tajiri angalia yasije yakakutokea puani. Ila kama hauna makuu ya kupoteza jichanue chap chap. Mimi natafuta kama hao niwape elimu ya investment. Yule aliye leta huo mchezo wa meli alicheza kama pele except finishing very poor. Hawa wazungu wanataka kufanya kwamba wa-iran kuwekeza hapa ni ubadhilifu wa hela. Simply kwa sababu hawatakiwi kuwa na uwezo wa ki vita.
 
wa Iran wako poa ila nikutahadharishe kitu

jamaa hawapendi urasimu na longo long ambazo ndio middle name za watanzania wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…