Ibrahim Quan
Member
- Jul 24, 2020
- 6
- 0
BIASHARA
Biashara ni nini?
Biashara ni makubaliano ambayo hufanyika bayana ya pande kuu mbili, muuzaji na mnunuzi, amabapo makubaliano hayo hufanyika juu ya bidhaa au huduma anayo itoa muuzaji. Makubaliano hayo pia hujumuisha thamani ya bidhaa au huduma hiyo. Au
Biashara ni kitendo cha kuuza na kununua bidhaa. Ikumbukwe kua biashara ya aina yoyote ni lazima ijumuishe pande kuu mbili ambapo upande wa kwanza ni wa muuzaji na upande wa pili ni wa mnunuzi. Muuzaji huuza bidhaa au huduma kwa lengo la kujipatia kipato au faida ila mnunuzi hununua bidhaa hiyo au huduma hiyo kwa lengo la kutimiza mahitaji yake au matakwa yake.
Sikuzote biashara ambayo imekamilika ndiyo biashara ambayo inafanikiwa. Vitu vikuu vinne ambavyo unapaswa kuvitambua katika biashara ni:
Ili biashara yoyote iweze kukamilika kunapaswa kuwepo na mahusiano mazuri,maelewano baina ya muuzaji na mnunuzi. Mfanya biashara yeyote kabla ya kufanya biashara anapaswa kutambua viashiria ambavyo ni vya lazima kuvijua ili biashara yako iweze kufanikiwa. Je unajua ni viashiria gania ambavyo vitakuonyesha au vitaonyesha biashara ambayo unaifanya au ambayo ulisha wahi kuifanya ilikua imekamilika au itakamilika? Kama ulikuwa hujui kuna viashiria vikuu sita ambavyo huashiria biashara iliyokamilika
Muuzaji, huyo ndiye mtu ambaye ameanzisha biashara, mtu huyu huuza bidhaa au huduma kwa wateja wake au jamii kutokana na uhitaji jamii hiyo inayomzunguka. Lengo la muuzaji ni kujipatia faida au kukuza kipato chake. Wajibu wa muuzaji ni kutambua uhitaji wa wateja wake na kutoa huduma bora na iliyokamilika. Mara nyingi muuzaji ndiye mtu ambaye hupanga bei na thamani kulingana na ubora wa bidha na gharama alizo zitumia ili kuipata bidhaa hiyo au kuitengeneza. Muuzaji ana uwezo wa kumfuata mnunuzi alipo au mnunuzi akamfuata muuzaji alipo. Muuzaji ambae hufanikiwa ni muuzaji ambae hutoa huduma bora kwa wateja au wanunuzi wake na ni mtu ambaye hufanya biashara kulingana na mabadiliko na mahitaji ya kijamii .
Mnunuzi(mteja), huyu ni mtu mwenye uhitaji na bidhaa au huduma ambayo muuzaji anaiuza kwa ajili ya mahitaji yake binafisi au kwa ajili ya familia yake au ndugu pamoja na jamaa. Wajibu wa mnunuzi ni kumkaribisha nakumpokea muuzaji kama muuzaji atakua amemfuata alipo. Wajibu wake mwingine ni kumfuata muuzaji mahali alipo kama muuzaji huyo hamfuati mnunuzi (kwenda katika ofisi au eneo la muuzaji). Wajibu mwingine wa tatu wa mnunuzi ni kukubaliana na bei ambayo ataitoa muuzaji au kukataa kulingana na ubora pamoja na viwango vya bidhaa hiyo au huduma hiyo. Mnunuzi anauwezo wa kufanya makubaliano na muuzaji na kupata punguzo la bei ya bidhaa anayoitaka. Katika kiashiria hiki kuna aina kuu mbili za mnunuz
Aina ya kwanza ni aina ya mnunuzi au wanunuzi wa moja kwa moja aina hii ya mnunuzi au wateja hujumuisha watu wote ambao ambao hununua bitdaa na kuitumia yeye, nikimaanisha kua aina hii ya mnunuzi inawajumuisha wanunuzi wote ambao watanunua huduma na kuitumia wao wenyewe kwa matumizi yao binafsi, maranyingi wanunuzi hawa huhitaji bidhaa iliyo bora na huduma bora kwa wakati sahihi ili kukidhi haja zao au maitaji yao. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unatoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine na kununua bidhaa na kuanza kuitumia wewe ni aina hii ya mnunuzi pia inamjumuisha mtu alie tumwa bidhaa na mtu Fulani au taasisi Fulani kwa ajili ya matumizi yao. Kwamaana nyingine haw ani wanunuzi ambao hununua bidhaa na kuitumia moja kwa moja
Aina yapili ya Wanunuzi ni waanunuzi wasio wa moja kwa moja haina hii ya wanunuzi hujumuisha wateja wote na wanunuzi wote ambao hununua huduma kutoka sehemu Fulani (kiwandani, soko, taasis, duka au sehemu nyingine yeyote anayoweza kupata huduma au bidhaa anayo ihitaji na kwenda kuiuza tena. Maranyingi au kwa lugha nyingine aina hii ya wanunuzi inajumuisha watu wote ambao hununua bidhaa na kwenda kuiuza tena kwa lengo la kujipatia faida au kusaidia watu au jamii Fulani.
Maranyingi aina hii ya wanunuzi hupenda kufanya biashara na wafanya biashara ambao wamekamilika, ambapo wana uhakika wa kupata bidhaa wanazo zihitaji kwa wakati sahihi na kwa gharama nafuu. Mfanya biashara yeyote ambae anakutana na wateja wa namna hii anapaswa kumpa na kutoa huduma sahihi kwa wakati na kumuuzia bidhaa hiyo kwa bei nafuu ikipendeza ili kumvutia Zaidi kwa bei ya punguzo pasipo kuhadibu au kwa kuzingatia gharama ulizo zitumia kutengeneza bidhaa hiyo au kuipata.
Aina ya tatu ya wanunuzi ni wanunuzi ambao hununua bidha kwa lengo la kutoa msaada au kusaidia jamii Fulani, aina hii ya wanunuzi maranyingi hununua bidhaa na kutoa kama zawadi au msaada kwa watu wanao wapenda au watu wenye uhitaji na bidhaa hiyo. Mfano wa aina hii ya wanunuzi inaweza kua mtu yeyote au taasisi yoyote ambayo inanunua bidhaa na kutoa bure kwa wahitaji mfano wazee, wajane au mashirika yanayo lelea Watoto yatima. Maranyingi aina hii ya wanunuzi wanapo fika katika eneo lako la kazi au biashara hununua bidhaa nyingi kwa wakati mmoja. Wewe kama mfanya biashara unapaswa kujua ni kwanamna gani unaweza uka wahudumia wateja wa namna hiii ili kuweza kuitangaza biashara yako.

- Muuzaji
- Mnunuzi
- Bidhaa au huduma
- Thamani

- Bidhaa au huduma, bidhaa au huduma, ndivyo vitu pekee ambavyo vinamkutanisha muuzaji na mnunuzi, pasipo bidhaa mnunuzi hawezi kwenda kwa muuzaji au muuzaji hawezi akamfuata mnunuzi. Najua unaweza ukawa unajiuliza bidhaa ni nini? Au huduma ni nini? Napia ukajiuliza ni kivipi huduma inaweza ikawa ni biashara. Nianze na bidhaa, bidhaa ni kitu chochote kilicho tengenezwa kutoka kiwandani na mnunuzi au muuzaji anaweza akakishika au akakiona mfano wa bidhaa ni sabuni, nguo n.k, ila huduma ni msaada ambao anautoa muuzaji, msaada huo unaweza ukawa wa moja kwa moja kwa mnunuzi au ukawa si wa moja kwa moja.
Mnunuzi hawezi akakaa na huduma kama alivyo kaa na bidhaa. Maranyingi huduma huwa ni ya muda mfupi au matumizi yake ni ya muda mfupi. Mfano wa huduma ni uuzaji wa vyakula na usafi wa maofisini. Wewe kama mfanyabiashara ukitaka kutambua kama biashara yako imekamilika au itakakamilika ni lazima uwe na bidhaa au huduma ambayo utamuuzia muhitaji au mteja na kujua mbinu za ushawuzi ili kuweza kumfanya mteja wako avutiwe na bidhaa au huduma unayo itoa
- Thamani ni gharama ya bidhaa au huduma ambayo muuzaji huiweka kulingana na ubora wa bidhaa au huduma anayo itoa. Mara nyingi katika biashara za sasa ni kwamba thamani ya bidhaa ni pesa. Lakini katika miaka iliyopita thamani ya bidhaa ilikua ni bidhaa, nikimainisha kua hawakuwa na pesa ila walikua wanafanya biashara kwa makubaliano na mabadilishano. Kwa mfano mimi nakupa karanga na wewe unanipa mahindi.
Thamani au gharama ya bidhaa huwekwa kulingana ubora wa bidhaa au gharama zilizo tumika kusafirisha bidhaa hizo kununua au kutengeneza. Ili bidhaa au huduma iweze kunununuliwa ni lazima mfanya biashara niki mainisha muuzaji akubaliane na mnunuzi kuhusu gharama au thamani ya bidhaa hiyo. Ila ikumbukwe kuwa thamani ya bidhaa au huduma muda mwingine hupungua na pia huwa na punguzo la bei. Endapo mnunuzi atakubaliana na muuzaji gharama na kulipia gharama ya bidhaa hiyo basi hapo ndipo biashara hufanyika au itakuwa imefanyika.
Upvote
2