SoC01 Biashara ndogo ndogo, zimewainua watu na kuwafanya wawe mtajiri Sana

SoC01 Biashara ndogo ndogo, zimewainua watu na kuwafanya wawe mtajiri Sana

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Jul 29, 2021
Posts
81
Reaction score
158
Ni kitu ambacho nimejiuliza kwa muda mrefu Sana. Ni watu wengi Sana wanafanya hizi biashara ndogo ndogo kama kuuza nyanya, duka, kuuza samaki,kushona nguo, na biashara nyinginezo za kijasiriamali. Je ni kwamba hizi biashara hazina faida? Lakini kama hizi biashara hazina faida mbona watu wanaendelea kuzifanya? Nadhani kutakuwa na changamoto na sababu nyingine ambazo huchangia wajasiriamali wadogo kutoweza kupiga hatua na kufanikiwa kupitia biashara zao.

Kwanza, hatuna imani ya kuwa hizi biashara: Nilimuuliza mtu ambaye aliyekuwa akifanya biashara ya kuuza ubuyu, sababu kuu ya kufanya biashara hii, alinijibu kuwa yeye huuza ubuyu ili aweze kutatua matatizo na kutimiza mahitaji yake madogo madogo, kama kulipia maji na kulipia umeme. Hii siyo sababu mbaya, ila ni sababu dhaifu. Na kama sababu ya kufanya Jambo lolote lile ni dhaifu, kufanikiwa katika hilo jambo Ni ngumu sana. Na hii ndiyo inayotokea katika katika wajasiriamali wadogo. Kama unafanya biashara yako labda ya kuuza mitumba au kuuza ubuyu kwajili ya kulipia umeme, hautaifanya kwa uzito mkubwa sana kama ungekuwa unaifanya ili ufanikiwe au ufike kwenye hatua fulani ya kimaisha.

Kudharau biashara ndogo ndogo: watu wengi hasa watu waliosoma wanatabia ya kudharau Sana hizi biashara, wanaamini kwasababu wamesoma na Wana degree au masters, kuuza mkaa, machungwa , ubuyu Ni kujishusha hadhi na haiendani na nafasi zetu.
Kuchukulia kuwa biashara ndogo ndogo Ni za kimasikini: Watu wengi hawapendi kufanya hizi biashara ndogo ndogo kwasababu wanaziona kuwa ni hizi biashara Ni za kimasikini na Ni za watu wasio na pesa, na walioshindwa maisha kabisa. Na ndio maana watu wengi huwa dharau sana mtu anayeuza mishkaki au machungwa barabarani na kumuheshimu na kumuona mtu aliye ajiriwa kuwa ndo mwenye thamani zaidi, kwasababu aliyeajiriwa anaonekana kuwa anapesa au amefanikiwa zaidi, kumbe ukija kuchunguza utakuta mwenye biashara ndogo huingiza kipato kikubwa kuliko hata aliyeajiriwa.

Hofu ya kuonekana na watu: Baadhi ya watu hasa vijana, tunashindwa kufanya biashara ndogo kisa tunahofu ya jinsi gani, majirani na marafiki watakavyo tufikiria, tunahofia tutaonekana tumeishiwa na tunashida Sana.

Tunasubiri kuajiriwa: Bado vijana tuna dhana ya kwamba tukisoma kwa bidii na kufaulu tutaajiriwa, badala ya kutumia elimu tuliyokuwa nayo kufanya biashara. Ukweli ni kwamba ajira ni chache na haziwezi na serikali haiwezi kuajiri kila kijana anayemaliza masomo yake, hivyo ni wajibu wetu sisi vijana kujaribu mambo mbalimbali hata biashara ndogo ndogo ili kujiendeleza.

Tunachelewa kuanza hizi biashara, Kuna kipindi niliwaza hivi kama ningeanza kufanya hii biashara wakati nipo mwaka wa kwanza chuoni, ningekuwa wapi? Ningeanza kuchukua hatua hii mapema ningekuwa nimepiga hatua kubwa sana. Ukichunguza utagundua kuwa watu wengi tunaanza baadae Sana unakuta mtu ana anza kufanya biashara ndogo ndogo baada ya kumaliza masomo na kuona maisha yalivyokuwa magumu mtaani, hebu fikiria kama mtu huyu angeanza kabla ya kumaliza chuo? Au unakuta mwingine anaanza baada ya kuwa na familia na kuwa na majukumu mengi. Kwa mtu kama huyu itakuwa ni changamoto kufanikiwa kwasababu faida atakayoipata hapo, itakuwa na matumizi mengi sana.

Tunafanya kwa kujaribu: Nadhani Ni sababu ya kutokuwa na elimu nzuri ya biashara, ndio maana watu hubadilisha biashara mara kwa mara. Akisikia biashara hii in pesa anaacha aliyokuwa anaifanya anaenda kwenye hiyo, akisikia biashara ya kuuza mishkaki ina pesa sana, anaacha kuuza matunda anahamia kwenye mishkaki. Katika biashara yeyote inabidi uwe mvumilivu, maana kwa mfumo wa kuhama hama hautaweza kuona faida yeyote.

Kukosa adabu ya pesa: Ukiwa unafanya biashara, hasa kwa biashara ndogo inabidi kiasi kikubwa Cha pesa kirudishiwe kwenye biashara, ili kuweza kuukuza mtaji wako. Lakini kinachotokea Ni kwamba huwa watu wengi tunatumia faida yote na wakati mwingine tunajikuta tunatafuna hadi mtaji. Hii inasababisha biashara zisiweze kuendelea kwa muda mrefu.

Wengi wetu tumezichukulia hizi biashara kuwa Ni biashara za kimasikini na zinafanywa na watu wenye shida, ni kweli , lakini pia hizi biashara ndogo ndogo, zimewainua watu na kuwafanya wawe mtajiri Sana. Nadhani changamoto inakuja katika imani uliyonayo kuhusu biashara hizi na jinsi ya ufanyaji wako.
 
Upvote 6
Back
Top Bottom