Samedi Amba LLC
Member
- Apr 5, 2024
- 81
- 117
Habari wanaJF,
Leo nimemaliza rasmi kazi yangu hapa Dar naelekea Moro. Mambo hayakuenda nlivyotarajia, lakini Inshallah, riziki ni ya Mwenyezi Mungu.
Baada ya kuachwa na treni miezi miwili ilopita, niliamua kuwa nkiwa natoka dar, nachukua treni ya mwisho. Inanipa muda wa eventualities na dharura za maisha. Na pia nasafiri kwa kurelax.
Nnaposubiri treni ya saa 12.55, nimeamua kujiegesha kwenye mgahawa wa TRC. Nlipokuwa napanda ngazi, nkaandamwa na jamaa mmoja. Muonekano wake ulikuwa kama mhudumu hivi.
"Habari kaka", akanichangamkia. "Salama aisee" nikasema, huku nashangaa kama TRC pia wanakuaga na matapeli. "Karibu sana Marafiki Restaurant". Asante. Anasema hivi, huku anaelekea restaurant ya TRC. Nkadhani TRC wamebadili brand, au la wameprivatize resturant yao.
"Kuna mtu namchecki hapo juu", nikasema kumpoteza. Akaniacha, akarudi kwenye ngazi.
Kumbe Marafiki Restaurant ni mpya na siyo ya siku nyingi. Nilipenda kidogo tactic yao ya kuchangamkia wateja, jambo ambalo TRC walikuwa hawajafanya vyema. Kuna siku nimekaa kwenye meza kwa zaidi ya dakika 40 hakukuwa na wa kunihudumia au kusogea niliko... Nikashangaa sana.
Leo, kaka kanisindikiza, na mhudumu wa TRC akaja kunikaribisha. Na naona wanaendelea kuwachangamkia wengine. Huenda, kuna wakati biashara inahitaji ushindani ili kuchangamka.
Na tujifunze KUUZA KILA SIKU. Na huwezi kufanya hivyo bila kutangaza biashara yako. Hakuna biashara isiyotoka bila matangazo.
Nlikuwa na jamaa jana (mkuu wa mafundi wa kompyuta kariakoo). Akaniambia hana haja ya matangazo wala mabango. Kwa kuwa biashara na network aliyoijenga inamtosha. Na sababu alizotoa zilikuwa za kueleweka.
Kuna wakati utafika mtandao wako utakubeba. Lakini kwa kuwa bado unajitafuta, tangaza ndugu. Endelea kuboresha. Tumia namna mbali mbali. Kwa kuwatafuta mmoja mmoja alivyofanya kaka.
Kwa kutumia Insta na FB. Kwa kutumia matangazo ya kulipiwa. Matangazo ya kubandika. Fanya chochote. Tangaza biashara.
Na yule jamaa wa kompyuta alianza kwa kutangaza. Alitengeneza A3 na kubandika pale UDSM akiwa chuoni. Ofisi ipo kwenye begi. Baadaye akaanza kuprint colored. Akafungua ofisi ya kwanza. Na ya pili. Na sasa anadhamiria kukodisha jengo nzima ili kuhudumia wananchi.
Tangaza biashara yako. Utanishukuru baadaye.