Elisha Chuma
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 282
- 275
Ili biashara ipate nafasi sokoni lazima kuwe na ushindani,ili mteja apate thamani lazima kuwe na ushindani hivyo hakikisha biashara yako ama wazo lako ni la kishindani na lina mbinu na uwezo wa kusimama kwa mpinzani wako.
Siku zote mshindani wako anaangalia makosa yako ili arekebishe ampate mteja wako ni kama kijiti kupokezana ila umuhimu zaidi unakuja pale ambapo ukimtengenezea tabia mteja wako unamjengea uaminifu,leo hii hata wewe mwenyewe kuna biashara ambayo imekutengenezea tabia na wewe umeipa uaminifu,hata kama iko mbali utaifata,hata kama itachelewa utaisubiri sababu ya kutengenezewa tabia na biashara yenyewe kwa kuwa na mbinu thabiti.
Unapowaza biashara yako leo hii anza kuwaza na ushindani wake lakini usiishiwe mbinu na kizuri zaidi soko huwa linabadilika siku kwa siku hivyo unapata nafasi ya kuongeza mbinu na kumsoma mshindani.
Heri ya mwezi mpya wa Disemba,tujiandae kwa majukumu ya januari bila kusahau..Malengo yako na mipango yako.