Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Wakuu mpo njema?
Swali langu ni kuhusu wafanyabiashara ambao wameweka kambi kwenye kituo cha daladala pale Kawe karibu na anapofanyia mikutano Mwamposa. Sasa hivi sehemu ile imejaa wafanya biashara wadogo (machinga) na mama ntilie wa kutosha. Mazingira ya hapo kweli hayaridhishi, ukiangalia jinsi walivyojipanga kukiwa na huduma ya choo imebanana hapo hapo karibu na mama ntilie wanaopika vyakula hapo lazima ujiulize kwanini iko hivi?! Lakini pia biashara zinafanyika karibu kabisa na barabara jambo ambalo linahatarisha usalama wao, gari ikiteleza kidogo tu na kuacha njia basi tutaingia kwenye msiba wa taifa.
Swali ni je, mamlaka zimetenga eneo hilo kwa wafanyabiashara hao kuendelea na shughuli zao kisheria, au ndio wanasubiri miaka miwili mitatu wafanya biashara hao wakiwa wamewekeza vizuri na kujimilikisha sehemu hiyo ndio waje na timuatimua kwamba eneo walilopo ni kinyume sheria? Kama wapo hapo kinyume na sheria kwanini wanaachwa kuendelea kuwepo hapo na kuendeleza biashara zao?