prumpeti
JF-Expert Member
- Feb 28, 2022
- 1,023
- 2,308
Habari za jumapili,
Leo nataka tuzungumze pamoja faida za kuwa mzalishaji wa kwanza wa bidhaa na kuingiza sokoni.
Ukweli ni kwamba biashara ndio muhimili wa uchumi wa Dunia, Serikali nyingi zina uchumi mkubwa kwa kufanya biashara. Leo tuangalie faida za kuingiza bidhaa sokoni ukiwa mzalishaji wa kwanza.
1. BEI
Unapokuwa mzalishaji unakuwa na uhuru wa kupanga bei ambayo haitakuwa na ushindani mkubwa sokoni tofauti na bidhaa za kununua na kwenda kulangua, hapa mara nyingi bei inategemea na ulivyo nunua.
2. UPEKEE
Linapokuja swala la ubunifu hapa ndio utakuwa umeula sababu ikiwa umebuni bidhaa kwa kuangalia uhitaji utapata soko kwa haraka zaidi na ndivyo faida itazidi kuwa nono.
3. UBORA
Kwasababu wewe ndio mzalishaji ni rahisi kuandaa kitu kizuri zaidi kuliko kununua bidhaa kutoka kwa mtu mwingine inaweza kukupa changamoto sokoni sababu wengi hawazingatii ubora hivyo mzigo unaweza ukakudodea..
MWISHO
Ushauri kwa vijana wanaotaka anzisha biashara wangalie zaidi kwenye kuzalisha kuliko kulangua...