Biashara nzuri ni ya uzalishaji, si ulanguzi

prumpeti

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
1,023
Reaction score
2,308
Habari za jumapili,

Leo nataka tuzungumze pamoja faida za kuwa mzalishaji wa kwanza wa bidhaa na kuingiza sokoni.

Ukweli ni kwamba biashara ndio muhimili wa uchumi wa Dunia, Serikali nyingi zina uchumi mkubwa kwa kufanya biashara. Leo tuangalie faida za kuingiza bidhaa sokoni ukiwa mzalishaji wa kwanza.

1. BEI
Unapokuwa mzalishaji unakuwa na uhuru wa kupanga bei ambayo haitakuwa na ushindani mkubwa sokoni tofauti na bidhaa za kununua na kwenda kulangua, hapa mara nyingi bei inategemea na ulivyo nunua.

2. UPEKEE
Linapokuja swala la ubunifu hapa ndio utakuwa umeula sababu ikiwa umebuni bidhaa kwa kuangalia uhitaji utapata soko kwa haraka zaidi na ndivyo faida itazidi kuwa nono.

3. UBORA
Kwasababu wewe ndio mzalishaji ni rahisi kuandaa kitu kizuri zaidi kuliko kununua bidhaa kutoka kwa mtu mwingine inaweza kukupa changamoto sokoni sababu wengi hawazingatii ubora hivyo mzigo unaweza ukakudodea..

MWISHO
Ushauri kwa vijana wanaotaka anzisha biashara wangalie zaidi kwenye kuzalisha kuliko kulangua...
 

Ungewambia hao vijana wazalishe bidhaa gani na kwa namna gani? Haya uliyoandika hayajatofautiana na singeli za WANAPOLITIKISI.
 
Mkuu inategemea unalangua bidhaa gani,kuna watu ni walanguzi na wanapiga hela ndefu kuliko wanaozalisha na hawana stress za kulipia rent na kodi za TRA.

Ofisi zao utawakuta wamekaa baa tu na Tablet/Laptop. Chukulia mfano mdogo tu madalali wa mazao utakuta mkulima amehangaika kwa muda wa mwaka au miezi 6 kuandaa shamba mwisho wa siku akivuna na kumuuzia dalali akitoa gharama zote alizotumia unaweza kuona anapata faida kidogo sana kwa kila gunia moja wakati huo dalali anaenda mashambani anachukua gunia moja kwa elfu 40 anaenda mjini kuuza elfu 80 ndani ya siku 1 au 2 ameshamaliza anaweka hela mfukoni.
 
Ungewambia hao vijana wazalishe bidhaa gani na kwa namna gani? Haya uliyoandika hayajatofautiana na singeli za WANAPOLITIKISI.

Sasa huo ni uvivu wa kufikiri kila kitu afanyiwe, hapana siyo sawa. Wa kufanyiwa kila kitu hawezi kuwa mfanya biashara
 

Hapo inategemea malengo ya biashara kama kwaajili ya kupata hela ya kula leo sawa ila kama unataka kukuwa kuwa mkubwa ni bora kuwa mzalishaji.
Kikubwa kuchagua nini cha kuzalisha kitafutie upekee kita kupa matokeo Mazuri.
 
Hapo inategemea malengo ya biashara kama kwaajili ya kupata hela ya kula leo sawa ila kama unataka kukuwa kuwa mkubwa ni bora kuwa mzalishaji.
Kikubwa kuchagua nini cha kuzalisha kitafutie upekee kita kupa matokeo Mazuri.
Haya ni mawazo ya kukariri mkuu,ukiingia field kwenye uhalisia mambo hugeuka na kuwa kinyume.

Your statement is true if you are in the level of Aliko Dangote, Mo dewji,Yusuph Manji, Bakhresa. Lakini kama uko viwango vya small scale & medium scale,you are wrong.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…