Biashara ya AGROVET (KUUZA PEMBEJEO ZA KILIMO NA MIFUGO)

Joined
Mar 4, 2020
Posts
12
Reaction score
21
Habari wa WADAU
Naitwa Mr. t
Nilikuwa ninawazo la kuanzisha biashara ndogo ya agrovet Kuuza pembejeo za kilimo na mifugo mtaji wangu ni 2.5 m hapo nihela ya mzigo tu.
Dhumuni langu Nini.
1.kuna wadau humu wanajua ABC's za izi biashara
A)chimbo la bidhaa
B)mambo ya vibali ila ningetamani kuanzia rural ambapo sitakuwa nahaja na licenses zozote na vurugu za TRA
C)Sheria na kanuni za hii biashara.
2.LOCATION YA BIASHARA
Kwangu Mimi nilikuwa nimependelea mikoa ambayo kilimo kifanyika na pia watu Wana mifugo ya kutosha ili kuwa na uhakika wa mzunguko
Maeneo niliyo yapa kipaumbele ni
1.mkoa wa katavi na wilaya vijiji vyake
2.geita
3.morogoro
4.rukwa
Tafadhali tusaidiane mawazo WADAU karibuni ....
 
Naona kila kitu umeshapanga labda chimbo tu la kupata bidhaa,bidhaa utapata kwa wauzaji wakubwa wa mikoani ambapo wew kwenye kila bidhaa utaongeza pesa itakayo kupa faida na kurudisha gharama zako za uendeshaj wa hyo kazi

Hii biashara inausumbufu sana kwa watu wenye mamlaka ukiachana na hao wa TRA lakin ajabu kila siku watu wanaanzisha kwahyo usiogope
 
Biashara nzuri, lakin hii biashara inawalenga zaidi watu chini maana kilimo na ufugaji kwa kiasi kikubwa kinafanywa na watu wa chini(walioko vijijin na hawana elimu kubwa sanaa) hivyo basi tafta eneo ambalo utaweza kuongea nao kabila Moja hii itarahisisha mawasiliano.

Rukwa sikushauri.
 
Enxs much bro.
 
Sawa.. kwanini si rukwa mkuu. Sababu ata mie sio mwenyeji wa hayo maeneo niliotaja ila natamani nisifanyie nje nyumbani.
Pia sio lazima biashara ya agrovet hapana nachojua me natamani nifanye kazi yeyote ambayo hataingiliana Moja Kwa Moja na vibali vya serikalini sababu mtaji Bado ni mdogo Mimi ni graduate wa kilimo na mifugo ila saizi Nina kazi ya mkataba kwenye kampuni binafsi na nimeweza kufanya kazi kwenye watu binafsi wengi sana.. sasa natamani nifanye changu niache kutegemea salary kama main income afu
Niko very competent skilled kwenye vitu vingi vya field yangu..
Plan B kama agrovet hatawezekana
1.biashara ya bucha
2.kilimo Cha bustani nyanya na vitunguu
3.kiwanda kidogo Cha bidhaa zamaziwa
4.ufugaji wa kuku chotara au nyama
NB.nita adjust mtaji kulingana na gharama za mradi.
 
we upo mkoa gani
 
Nitakuelekeza kwa urefu zaid mkuu.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ yawezekana wadau hawana deep data kuhusu hii biashara dahh inanibidi niingie ivoivo ndo nitajifunza zaidi... Nikiwa field..
 
Demand kubwa ipo kwa Sasa Dodoma!
 
Kila la heri mpambanaji mwenzangu
Hapa sitatia neno maana Sina uelewa sana na hii biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…