Biashara ya aina moja au diversification?

nyabaheta

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
247
Reaction score
82
Wadau habari zenu
Kuna jambo moja linanitatiza wakuu nimeona nililete kwenu,mimi najihusisha na biashara ndogondogo,nimekua njia panda juu ya nini cha kukifanya mara nipatapo faida,ipi approach nzuri,niendelee kuwekeza katika kuikuza hiyo biashara ndogo au niwekeze kwenye biashara zingine pia(diversification).
Kwa uzoefu wenu na utaalam,ipi bora?

Nothing comes to a sleeping man but dreams-Tupac Shakur
 
Mkuu kwenye biashara kuna neno moja tu lenye maana (FAIDA), kwahio wewe angalia opportunity cost na ni biashara ipi shilingi yako inazaa maradufu wewe fanya hio, na kama pesa ipo wekeza kwenye biashara zozote so long as kuna profit.

Hakikisha umefanya homework yako na unajua unachokifanya. Faida ya diversification ni kupunguza risk kwamba biashara hii ikikataa ile itakubali lakini kama ukizifanya bila uzoefu hakika ninakwambia zote zitakataa (hapa ndio msemo wa stick to what you know unakuja., na ukihamia pengine hakikisha una-knowledge ya unachotaka kufanya)
 
Nimekusoma vyema mkuu sun wu.

Nothing comes to a sleeping man but dreams-Tupac Shakur
 
Unaweza uka diversify kama una mtu muaminifu e.g. mke wako anakusaidia katika hizo biashara. Ila kujigawa mwenyewe sehemu zaidi ya moja i.e kwa biashara zaidi ya moja bila mtu makini wa kukupa msaada ni ngumu kufanikiwa. Kwa maana, mtaka yote kwa pupa hukosa yote au more correctly.....Mshika mawili moja humponyoka
 
Mwafrika usema "Do not put all your eggs in one basket" Naye mzungu usema
"put all your eggs in one basket and watch that basket"

unapenda lipi?
 
Mwafrika usema "Do not put all your eggs in one basket" Naye mzungu usema
"put all your eggs in one basket and watch that basket"

unapenda lipi?

Mkuu hiyo ID yako vipi? au ndo mambo ya wachina?
 
Mwafrika usema "Do not put all your eggs in one basket" Naye mzungu usema
"put all your eggs in one basket and watch that basket"

unapenda lipi?

Umeiweka vizuri sana mkuu,binafsi nilikua napenda hiyo ya mzungu,na nadhani hiyo ya mwafrika inatokana na kufanya mambo pasipo kujiamini,kwa hiyo wengi huishia kubahatisha.

Nothing comes to a sleeping man but dreams-Tupac Shakur
 

Mkuu kwani Business plan yako inasemaje? Vipi VISION NA MISON ya Biashara yako? Ulipo anza hiyo Biashara Lengo lako lilikuwa ni nini?

That is a problems to most of Business man hapa Bongo, Nakumbuka kuna mzee mmoja ni Mfanya biashara Anamiliki Gest, ana kibanda cha kuchajisha simu na ana miliki Bodaboda, kuna day nika muuliza Mzee lengo hasa la Biashara yako ni nini? Vipi unataka siku moja uwe wapi? kwa kweli majibu ya yule mzee yalikuwa ni ya kusikitisha,

Watu wengi sana tunafanya biashara bila Malengo au Taget, That is why utakuta Mtu ana Gest, ana Basi, Ana Ngo'ombe wa Maziwa na kazalika, sasa unashindwa kuelewa VISION ya huyu mtu ni Ipi Hasa?

Kuwa na Biashara Nyingi inawezekana Ila ni Kwa Makampuni Makubwa ndo wano fevwa na hii kitu inayo itwa SBU,(Startegic Bunsiness Unit) na kuna kitu kinaitwa BCG(Boston Consulting Group) so unapo kuwa na biashara kama nne maana yake zinakuwa zinategemeana yenye kutoa faida kubwa inanyanyua hizo zingine,

But SBU inafeva biashar kubwa ambazo unakuta zinauzoefu mkubwa, Na managment inakuwa isha kuwa kubwa na uzoefu wa kufa mtu, Chukulia mfano wa SUMSUNG, Wana Mafrdge, Simu, Radio, Komputer so hiizi mara nyingi kwenye kampuni zinakuwa zinategemeana, Frdge wanaweza kuwa wanafanya vizuri sana so sehemu ya Faida yao inaenda kugaramikia utengenezaji wa Computer
,

so ni bora mkuu ukawa na VISION yako na Madhumuni ya wewe kuingia katika biashara ni yapi? unataka kuwa wapi miaka kadhaa ijayo? na kazalika

Na Mara nyingi unatakiwa kutengeneza SBU unapo kuwa umesimama na biashara yako isha weka mizizi kabisa kiasi kwamba una watu wakutosha kuendesha hiyo SBU
 
aha ha! mkuu, chash na chasha nitofauti sana, ni kama car na care, utasema car ni kichina ya care?

No mkuu katika kusajili majina kuna sheria zinazo ongoza mfano mambo ya Phonetic, so hapo ukija kwenye Phonetic na too like hairuhusiwi wewe kutumia hilo jina

Mfano: Charls Comapy Ltd haiwezi kusajiliwa kama kuna Charles Compay LTD,
 

No mkuu katika kusajili majina kuna sheria zinazo ongoza mfano mambo ya Phonetic, so hapo ukija kwenye Phonetic na too like hairuhusiwi wewe kutumia hilo jina

Mfano: Charls Comapy Ltd haiwezi kusajiliwa kama kuna Charles Compay LTD,

Lawama ni kwa msajili wa majina au ni kwa applicant? unapo omba kusajiliwa huna record ya walio tangulia usajili. Hiyo huwezi jua hadi baadaye, kama sasa tunagundua kuna mtu ameiga jina langu alafu aka backdate
 
Si vema kufanya diversification kabla hujaimarisha biashara yako ya msingi, kumbuka kupata faida mara moja ama mbili haimaanishi kuwa biashara yako imeimarika. Make sure biashara yako umeimarika kiasi cha kutoweza kuyumba panapo defaults ndogo ndogo, hakikisha umejifunza mengi juu ya biashara yako ya sasa na unamtandao wa kutosha kibiashara.

Pili si vema kuingia katika biashara zingine kwa kusikia tu kuwa zinalipa sana ama kuhamisha mtaji. Hakikisha kwanza umeifahamu kiundani biashara hiyo mpya na uhamishaji huo wa mtaji hautaathiri biashara yako ya sasa.

Tatu kuna changamoto kubwa ya usimamizi, je umejiandaa kuweza kusimamia project zaidi ya moja? Na hapa ndipo wengi panapowashinda maana unaweza ukajikuta kwa ufanisi mdogo wa kuweza kufuatilia kwa karibu miradi yote ukaingia hasara kubwa na pengine kupoteza kila kitu. Ningekushauri tu kwanza jenga himaya yako katika biashara yako ya sasa kabla ya diversification.
 
hapana nakushauri bora uendelee na hiyo biashara yko.hio faida unayoipata jaribu kuirudusha as capital,ukiendele hivo ni rahisi sana kukuwa.pili ukijaribu kufanya kitu kingine ni rahisi sana kuangua kwamfano ikitokea tafauti na matarajio yako ie loss piya muda wako mwingi utaweka ktk hio biashara mpya so ile ya mwanzo inaweza kuyumba.sio hayo tu hata cost itaongezeka kuliko kuikuza biashara ya mwanzo.so its better u pull ur profit so as 2 grow ur business may b afterwards u wll think abt diversifng but for no...
 
Mwafrika usema "Do not put all your eggs in one basket" Naye mzungu usema
"put all your eggs in one basket and watch that basket"
UT ALL YOU EGG IN ONE
unapenda lipi?
KAKA NIMEIPENDA HII YA `"Put all your eggs in one basket and watch that basket"
 
Mwafrika usema "Do not put all your eggs in one basket" Naye mzungu usema
"put all your eggs in one basket and watch that basket"

unapenda lipi?

Mkuu huo msemo "do not put all eggs in one basket" ndo unaotumika na wadhungu kwa sana.
 
Mkuu huo msemo "do not put all eggs in one basket" ndo unaotumika na wadhungu kwa sana.

Hata hivyo ukiangalia top matajiri wa ulimwengu utapata ni walio specialize na biashara moja na kama utapata amewekeza kwenye shughuli nyingine ni ile inaongeza nguvu kwenye main business. Hiyo ya 'don't put all your eggs in one basket' inatokelezea kuwa 'Jack of all trades and master of none'
 
Mkuu hakuna tatizo kabisa! Kimsingi mafanikio yeyote katika biashara yanategemea sana usimamizi mzuri. Iwapo utajipa muda wa kutosha kufuatilia kwa ukaribu na kuzisimamia vyema, unaweza kuwa na biashara hata zaidi ya kumi na mambo yakawa Super tu!
 
According to Warren Buffet: During Investment...Do not put all eggs in one basket....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…