Biashara ya Alzeti

Einsten

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2013
Posts
921
Reaction score
795
Kama kichwa kinavyojieleza naomba mwongozo wa upatikansji wa alzeti maeneo ya singida najua humu kuna watu wanafanya hii biashara.
Nilitaka kujua mtaji wa below 3M unatosha kuja nayo huko kama nitapata profit?
 
Kwa sasa hupati alizeti hata wakati wa mavuno ukifika mid june hadi july watauza bei ghali sana na wengi hawatauza watazitunza ndani.

Alizeti imewapa hasara wakulima kama misimu mitatu mfululizo hivyo huu msimu wamelima kidogo mno kwa maeneo nayoyajua na yana hadi viwanda vya alizeti vikubwa
 
Upo sahihi kweli alizeti imewapa watu hasara zaidi ya miaka mitatu
Lakini iyo sio sababu itakayo fanya wakulima wasiuze alizeti pindi watakapo vuna

Ipo ivi wakulima wengi wa Singida vijijin wanasema zao la Alizeti linawasha [emoji1787][emoji1787][emoji1787] wakimaanisha aitunziki kama Mazao mengine kwa sababu pesa yake ipo njenje sio kama Mazao mengine maana alizeti aina dalali kwa upande wa Singida vijijin ivyo wakulima wengi wanauza pindi wanapo vuna pia hubakisha kiasi kidogo ili kuja kuchanganya na Alizeti pori (Katamu)

Pia wakulima wengi huwa wanachukua advance kutoka kwa wateja wao ivyo atakavyo vuna tuu inabidi auze iyo Alizeti yake kwa mteja ambaye alimpa advance
 
Kama kichwa kinavyojieleza naomba mwongozo wa upatikansji wa alzeti maeneo ya singida najua humu kuna watu wanafanya hii biashara.
Nilitaka kujua mtaji wa below 3M unatosha kuja nayo huko kama nitapata profit?
Hongera kuwa na wazo kama ilo Mkuu

Mambo ya kuzingatia ili uweze kununua Alizeti yako ni kama yafuatayo


✓ Unanunua kwa ajili ya Nini

Kama Unanunua kwa ajili ya kuuza iyo Alizeti pindi itakapo panda bei basi usisumbuke kununua Alizeti kutokana na aina (Variety) ww nunua variety yoyote ile lkn hakikisha imepetwa vizuri ayo mengine atajua uyo mtu utakaye muuzia

Kama Unanunua kwa ajili ya kukamua mafuta basi zingatia Mambo ya fuatayo

1.usinunue alizeti iliyo vunwa kwanzia mwezi wa 4 au 5 maana huwa inakuwa mapepe kwa sababu imevunwa kipindi Cha mvua ivyo ukienda kukamua utapata hasara maana kile kiini Cha mafuta kinakuwa kina maji na sio mafuta

2. Jitaid usinunuwe alizeti ile nyeusi ya kienyeji maana huwa inatoa mafuta kidogo ivyo utapata hasara lkn ukununua alizeti izo nyinge kama pundamilia, nyeusi yenye michilizi na ile kijivu basi utapata faida maana zinatoa mafuta mengi ( siwezi kusema ni Variety gani kwa jina lake maana nitakuwa nachafua biashara za watu ivyo kusema langi ya Alizeti inatosha Mkuu)

3. Jitaid kukamua kwanzia mwezi wa 8 hadi wa 10 maana kipindi kama hicho Jua huwa Kali ivyo ukianika alizeti yako itakauka vizuri ivyo mafuta yatatoka mengi lkn kama ukikamua mwezi wa sita mafuta yatatoka kidogo ata kama ukipata alizeti inayo toa mafuta mengi hii kutokana na miale ya Jua inakuwa sio mikali ivyo inapasha Alizeti kwa kiasi kidogo

4. Kabla ya kukamua ni vyema kumuuliza operator wa machine ni muda gani umepita toka achome shaft yake maana kama ijachomwa kwa muda mlefu ufanisi katika ukamuaji wa mafuta utakuwa mdogo ivyo mafuta yatatoka madogo kwaiyo apo inabid uwe makini Mkuu

5. Baada ya kukamua alizeti yako hakikisha mafuta unayo pewa ni Yale yalio toka kwenye alizeti yako kwa sababu Kuna alizeti pori ambayo huwa inakamuliwa kwa kuchanganya na Alizeti ya kwaida lkn mafuta yanayo patikana apo huwa ni machungu nakupelekea kiungulia yani kukeleketa kwaiyo endapo ukipewa ayo mafuta wateja wako wote watakukimbia Mkuu ivyo jitaidi kuchukuwa mafuta uliyo kamuwa ww ingawa inachukuwa muda wa 45 dakika kuchuja mafuta ivyo itabid usubili lk ukiwa na haraka itakula kwako

6 utakavyo enda kukamua alizeti yako inabid uacha liter 1-1.5 za mafuta kwa operator maana huwa yanapotelea kwenye filter ivyo usiache zaidi ya icho kipimo kwa kila gunia LA alizeti lenye 70 kg

✓ Namna ya kununua Alizeti. Nenda kwenye center au vijiwe vya kijijin kisha tangaza kwamba unanua alizeti kwa gharama flani na kipimo flani lkn jitaidi kutumia watu wa vijijin ili wenyewe wakutafutie wateja

✓ Inabid ununuwe kwenye ujazo wa plastic Yan debe iyo ndio njia sahihi lkn ukinunuwe kwenye ujazo wa gunia utapata hasara maana nivugumu kujua kama amejaza kwa ujazo sahihi au lahaa

✓ kama utatumia mtu kununua Alizeti jitaid usimpe pesa yote kama ni 3 M basi mpe 500k Kwa awamu ya kwanza then akikamilisha inabid uchukuwe mzigo then unampa 500k ivyo itakuwa lahisi pia usitumie mtu mmoja tafuta ata watu 5 kwa sababu ndani ya mwezi mmoja tuu utakuwa umekamilisha mzigo wa pesa yako

✓ Ukitaka alizeti nyingi na kwa bei ya chini nenda kanunue kwenye vijiji ambavyo avina umeme kwa sababu wakulima wengi awapendi kutafuta Masoko ivyo ww ukienda kununua uku utakuwa kama mkombozi wao maana watakuwa awana sehemu ya kuipeleka ivyo utapata mzigo wa kutosha na bei ambayo unaweza kuipanga wewe

✓ kila plastic au debe 6 inabidi umpatie uyo mtu ambaye anakununulia alizeti kiasi Cha 1000 au 1500 iyo ni kama motisha maana wateja wataleta alizeti nyumbani kwake ivyo iyo pesa inatosha kabisa

Kila lakheri Mkuu
 
Mungu akubariki Mkuu
 
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Lo....ingawa mhitaji siyo mimi, walakini ni vema na busara kupata majibu haya kutoka kwako. Ahsante sana kwa kujali na kwa muda wako mkuu, naam ubarikiwe kwa elimu na ujuzi uliotoa.
 
Kama ukikamua ukatoa mafuta yasiyoa harufu kama golden harvest, mount meru nicheki nikuunganishe na wanunuzi
 
Mungu akubariki sana ndugu! Mimi nilitaka nikanunue hii inayovunwa sasa hv ili nizungushie kwanza capital ili mwez wa 6 ndio nikanunue nying na mm lengo langu ni kununua na kukamua na kuuzia hapo hapo sitak stress za kuanza kusumbuana na madalali. Changamoto ya kukaa na vitu imenipiga sana kwenye mahind na mpunga.
 
Nilikuwa nauliza tena ndugu vipi hii alzeti mpya iliyovunwa mwez huu wa 4 siwez kutoa lita 20 kwa gunia moja??
 
Muongozo mzuri.
 
Nilikuwa nauliza tena ndugu vipi hii alzeti mpya iliyovunwa mwez huu wa 4 siwez kutoa lita 20 kwa gunia moja??
Kama nilivyo eleza apo juu Mkuu
Kupata mafuta mengi kwenye gunia la 70 kg inategemeana na vitu vingi kama vile
✓Aina ya Alizeti

✓ Ujazo wa gunia

✓Ubora wa machine

✓ Alizeti imevunwa kipindi gani

kama imevunwa mwezi wa nne unaweza kupata izo liter 20 kwa gunia endapo ukinunua alizeti kwenye mikoa ambayo ijapata mvua kwenye mwezi wa tatu kama vile singida lkn ukinunua kwenye ile mikoa ambayo imepata mvua mwezi ya 3 basi uwezi pata liter 20 kwenye gunia la 70 kg
 
Kama kichwa kinavyojieleza naomba mwongozo wa upatikansji wa alzeti maeneo ya singida najua humu kuna watu wanafanya hii biashara.
Nilitaka kujua mtaji wa below 3M unatosha kuja nayo huko kama nitapata profit?
Mkuu it's possible mfano mwaka huu msimu wa mavuno unaanza April mwishoni kwa singida vijjn na iramba Ila Ikungi ni may kwenye tarehe 10 hivi.
Hiyo hela inatosha kabisa Kama gunia hata lilianzia laki 1 unaweza kununua Magunia 25 na ukayapeleka kiwandani ukakamua ukapata faida .ukarudi Tena within a week

Ila zingatia ubora wa mbegu unazonunua,kuwa makini na ujazo (Gunia la alizeti huwa linashindiliwa haswa).
Kuwa makini kiwandani usibadilishiwe mbegu ama mafuta.
Kwa mtaji huo ingia vijiji vya Ikungi kuanzia Chungu,Nduru,Mtavira,Minyughe,Daraja,Magweghana etc
Huko Kuna vimizigo vidogo dogo vingi.
Uwe mwaminifu sana
 
Hiyo namba sita sijakupata vyema.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…