wana jf naangalia uwezekano wa kuanzisha biashara ya soko la asali katika soko la afrika mashariki hususani kenya.asali hii inapatikana kwa wingi tabora,shinyanga na dodoma.pengine kuna mwenye idea juu ya biashara hii,je inalipa?japo watanzania tu woga wa kuthubutu kuingia.
Asali organic kwa sasa unaweza kuipata maeneo ya Kondoa,Kigoma,Chunya,Iringa hasa wilayani kilolo. haya ni maeneo yasiyoathiriwa na kilimo cha mashamba makubwa yanayotumia dawa za kuulia wadudu.Hii asali ya Tabora si ndo ile waziri aliyo sema imekataliwa kwenye soko la Ulaya, na wauzaji wengi kwa sasa wameshindwa kupeleka kule kutokana na maswala ya ubora,
Hii asali ya Tabora hasa maeneo wanayo lima tumbaku imekuwa ikikutwa na nicoteen, hali ambao imesababisha nchi za ulaya kuikataa, na hii ni kutokana na uhalibivu mkubwa sana wa mazingira unao pelekea nyuki kuto kuwa na maua ya kutosha ya kutengenezea asali hivyo kurazimu kuchukua hadi ya Tumbaku,
Ila kwa huku Africa mashariki si dhani kama kuna tatizo so unaweza uza
Mkuu hongera kwa kuchagua njia hii. Biashara hii inasoko sana, but sokoni inahitajika asali bora na si bora asali. Ubora unapatikana kutokana na namna nyuki wanavyofugwa, vifaa unavyotumia na jinsi unavyorina. Suala la packaging, branding na TBS approval nalo ni la msingi pia. Watembelee African Beekeepers Limited utajifunza kitu kwenye soko hili.
Kila la heri
Asali organic kwa sasa unaweza kuipata maeneo ya Kondoa,Kigoma,Chunya,Iringa hasa wilayani kilolo. haya ni maeneo yasiyoathiriwa na kilimo cha mashamba makubwa yanayotumia dawa za kuulia wadudu.
Tufanyeje sasa?
Kuzalisha na ku-park mwenyewe ni bora zaidi kwa sababu unaweza kudhibiti ubora. Hili la kununua kwa wadau ni tatizo sana, chakachua imeingia kila kona.