Wakuu habari zenu.
Kwa muda mrefu nilikuwa na ndoto ya kufanya biashara ya asali, hapa Dar
ila bado ndoto yangu haijafanikiwa kwa kukosa mtaji wa biashara. Kwa
Dar peke yake kuna soko kubwa sana kwa kupitia mikakati ya masoko
niliyonayo kichwani.
OMBI LANGU:
Kwa kuwa mimi binafsi nimeshindwa kuwa na mtaji, naomba kama kuna mtu
ana mtaji au kama kuna mtu anafanya biashara ya asali na hawezi kupata
soko, naomba tushirikiane kwa makubaliano maalumu juu ya malipo kuuza
biashara hiyo, au kama unamtaji unaweza ukatoa mtaji mimi mimi
nikasimamia hiyo biashara na kisha faida tukagawana kwa makubaliano
maalumu.
Mimi nipo DAR kwa maelezo zaidi na mawasiliano ni PM.