Biashara ya Bar

Biashara ya Bar

Eddy Elphazi

Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
8
Reaction score
9
Habari wana JF. Nimekuwa nikifanya biashara ya grocery kwa mda sasa sema changamoto kubwa ninayokumbana nayo ni wingi wa madeni(nadai wateja), sasa nikawa nafikiria pengine nikihama eneo na kujipanua nikaanzisha Bar ya kawaida maybe ntakuwa nimesolve hii ishu ya kukopwa sana. Kama kuna mtu ana experience na hii biashara(Bar) ushauri wenu tafadhari🙏
 
Habari wana JF. Nimekuwa nikifanya biashara ya grocery kwa mda sasa sema changamoto kubwa ninayokumbana nayo ni wingi wa madeni(nadai wateja), sasa nikawa nafikiria pengine nikihama eneo na kujipanua nikaanzisha Bar ya kawaida maybe ntakuwa nimesolve hii ishu ya kukopwa sana. Kama kuna mtu ana experience na hii biashara(Bar) ushauri wenu tafadhari[emoji120]

Mkuu, pole kwa changamoto..
Ishu ya madeni kwenye biashara hasa Glocery ni tatizo kwa wengi wanaofanya biashara hiyo.

Kwa maoni yangu tatizo linaanza pale mahusiano/mazoea na wateja yakivuka mipaka, wengi watagugeuka wakishakopa watakukimbia na utakula hasara.

Cha kufanya ni kuzuia kukopa kwenye biashara hasa kwa marafiki, bora akuombe pesa umkopeshe ila sio kukopesha mtaji wa biashara. Akiamka asubuhi hangover ikiisha anajutia kwa kukopa na hafikirii kuirudisha.

Bar ni nzuri, ila customers utawapata ukiwa mbunifu.
1. Location
2. Wahudumu wako
3. Manager mwenye experience
4. Daily reconciliation ya mauzo na matumizi
 
Back
Top Bottom