Biashara ya bodaboda vs biashara ya duka la nafaka na mahitaji ya nyumbani

Ubungo Mataa

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2018
Posts
411
Reaction score
725
Wanabodi.. Heshima mbele!

Moja kwa moja kwenye msada, kuna 10M iko mahali, nawaza niiweke wapi kati ya kununua bodaboda nne niwape watu wakuleta hesabu kwa siku/ week ama nifungue duka ambalo roughly litakuwa kama la 8M maana 2M itaendwa kwenye running cost na kodi.

Msaada!
 
Inategemea na uwezo na uwezo wako wa kuzisimamia kwa umakini.
 
Ushauri wangu Ni huu;

Niliwahi kumiliki bodaboda mwaka Jana,wiki ya kwanza alinipa vizuri 70k yangu,wiki ya pili vikaanza visingizio,Mara juzi nilikuwa naumwa mafua kwa hiyo bosi utanidai nakuongezea katika hesabu ya wiki hi. Unamkubalia Cha ajabu na hiyo wiki analeta visingizio tena,deni linazaa deni.

Haujapita mwezi Kuna mtu anakuja kuniambia "pikipiki yako nimeona Kuna madogo Kama watano wamepakizana wameipiga mtungo huo mwendo Kama ngiri anawahi shimoni. Jamaa nampigia anasema anaumwa kifua kampa mshikaji wake amletee hela. Miezi mitatu pikipiki imechakaa. Kwa kuona aibu maaana alinifuata mwenyewe nimnunulie bodaboda Hali tete mtaani,akaanza visingizio kibao anataka tuvunje mkataba,nikamuuliza Sasa wewe ndiye uliniambia maisha magumu nikununulie boda angalau upate hela ya kula na kijiwe ulisema unacho maana ulikuwa unapiga day worker boda za wanao,akajibu bosi me naona Kama Nina gundu maana chombo kinaharibika,madeni mengi,bodaboda zimekuwa nyingi kijiweni,hell hakuna. Akaniambia namleta ndugu yangu umkabidhi. Wiki ya kwanza huyo ndugu yake kavunja side mirror.

Ni mfano tu ndugu,na to make story short niliiuza kwa Bei ya hasara. Ila Kama umeipenda hii biashara Kuna ambao inawalipa,na nilichojifunza Ni kwamba ukinumua bodaboda usimpe kijana asiye na majukumu, au hawa wanyoa viduku na wasikiliza singeli...Mpe pikipiki yako mtu mzima mwenye familia aliyekomaa akili. Ataifanya kazi kwa bidii na nidhamu maana ndiyo itamfanya apeleke mboga na unga nyumbani. Mimi nilifeli katika hiko kipengere.

Kuhusu duka tatizo linaweza lisiwe mtaji. Una mtaji mkubwa sana. Kuna watu wanaanza na Duka na mtaji wa chini ya milioni mbili na wanatoboa. Kitu Cha kuzingatia ni location. Jamaangu niliyesoma nae ambae amefanikiwa kwenye biashara ya viatu alinipa ushauri kwamba usione watu wanalipia fremu Hadi milioni ukawaona hawana akili,location Ni mtaji mkubwa kwenye biashara kuliko pesa,Kuna sehemu unakutana na fremu nzuri lakini hazina watu,ukiingia kichwakichwa na milioni kumi yako utalia kilio Cha mbwa. Fanya utafiti katika Hilo eneo utakuja kunishukuru.
 
Kufanya upembuzi wa aina ya mtu wa kumpa ni nzur ndugu binafsi nimeifanya 2016 m0ka 2019 nilikua nazo 10 Pikipik aisee nimejenga nyumba kali kwa hii kazi nasikitika tu nilipata changamoto ya kuibiwq nikaona nipumzike ila nataka nirud na kuzifunga gprs
 
Wanabodi.. Heshima mbele!

Moja kwa moja kwenye msada, kuna 10M iko mahali, nawaza niiweke wapi kati ya kununua bodaboda nne niwape watu wakuleta hesabu kwa siku/ week ama nifungue duka ambalo roughly litakuwa kama la 8M maana 2M itaendwa kwenye running cost na kodi.

Msaada!
Bodaboda kwa hesabu ndani ya siku/wiki utapata tabu sana na hao jamaa watakaokuwa wanaziendesha. Hasa kwenye habari ya service/maintenance. Binafsi nakushauri, fanya biashara ya bodaboda kwa mkataba. Mnaandikishana serikali ya mtaa. Hesabu ni 100,000/- kila baada ya siku 10 kwa kila bodaboda. Baada ya miezi 12, bodaboda inakuwa ya yule uliyeingia naye mkataba. Sehemu ya masherti ya mkataba ni kama ikiibiwa, au akishindwa kuleta hesabu ndani ya siku fulani Mtakubaliana) basi amevunja mkataba. Mnapiga hesabu ya muda uliobaki na hela ambayo ameshakupa againsta bei ya bodaboda ikiwa dukani. Then mnafikia jinsi ya kulipana.

Kama utahitaji sample ya mkataba njoo inbox
 
Kama utahitaji sample ya mkataba njoo

Habari mkuu? Nimeshawishika, Naomba sample ya mkataba na mimi nione
 
Back
Top Bottom