Biashara ya bodaboda

Kijana Mpole99

New Member
Joined
May 9, 2021
Posts
3
Reaction score
5
Habari Wakubwa,

Mimi ni Kijana ambae nimeamua kuanza kujiajiri,nimefanikiwa kupata hela ya kununua bodaboda boxer ambayo nitaendesha mwenyewe.

Naombeni ushauri wowote Au namna ya kuendesha business hii (faida,changamoto)

Natanguliza shukurani..
 
Duuh
Huenda humu ndan hakuna watu wanao jihusisha na Biashara hiyo
 
Habari Wakubwa,

Mimi ni Kijana ambae nimeamua kuanza kujiajiri,nimefanikiwa kupata hela ya kununua bodaboda boxer ambayo nitaendesha mwenyewe.

Naombeni ushauri wowote Au namna ya kuendesha business hii (faida,changamoto)

Natanguliza shukurani..
Hongera sana Dogo!
BODA BODA, ukiwa una endesha mwenyewe ni moja kati ya biashara NZURI SANA,
mimi nime ifanya Tangu nasoma form.6, chuo kikuu, Mpaka siku napata AJIRA Serikali Kuu.
Nime Somesha wadogo zangu wa.4 mpaka vyuo, kwa Boda boda.....!!
Angalizo;
1. Usiwe na Tamaa (Mademu ukiwa mzembe utakula mpaka ufilisike)
2. Uwe na NIDHAMU ya Fedha na KUWEKA AKIBA, (Elf.20 kwa siku ni uhakika)
3. Uwe makini Barabarani Kwa kufuata Sheria zote za USALAMA BARABARANI
4. Uwe Msafi, Mwaminifu na mwenye Kauli NZURI KWA WATEJA (Hii itakupa hakikisho wa wateja, Utatafutwa Popote ulipo na Utafurahia sana Kazi, mpaka wenzako wata kuonea WIVU)
5. Usiwe mvivu, pikipiki yako Endesha wewe mwenyewe siku zote. (Hii itakusaidia kuwa na Utunzaji wa Mali yako)
6. Piki piki ikiharibika REKEBISHA KWA WAKATI (Hii itakupa hakikisho la Uimara wa pikipiki yako popote na wakati wowote)
7. Uwe na Muda mzuri wa kupumzika (kulala na kuamka) Hii itakupa ratiba nzuri na wateja wako kuiheshimu, na KUEPUKANA NA WIZI wa pikipiki
8. Hakikisha Una Kula kwa wakati sahihi MLO KAMILI na Kunywa Maji Mengi, (Hii itakusaidia kuondokana na Uchovu na homa homa na UTUNZAJI WA AFYA YAKO)
9. Vaa mavazi SAHIHI ya pikipiki e.g Helment, Viatu, Jacket, gloves n.k (Hii itakulinda na Afya yako e.g UPEPO na Ajari hata kama ikitokea kwa Bahati Mbaya USIDHURIKE SANA)
10. Muombe Mungu kwa Imani yako kila wakati, Ili alete wateja na kukulinda.

Nakutakia kazi njema, na Mungu awe nawe,
HIZO NI CHACHE KATI YA NYINGI NILIZO KUWA NA TUMIA BINAFSI ZIME NI SAIDIA SANA
waweza kuongezea na zingine na kupata USHAURI TOFAUTI TOFAUTI.....!

Asante; na kila la kheri.
 
Ushahuri mzuri sana huu..

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante nashukukuru sana
 
Hongera kwa ushauri mzuri.kwenye app hizi mfano bolt , uber e.t.c ipi ni nzuri kwa pikipiki? Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…