Biashara ya Bodaboda

WATU KAKA TUNATAFUTA ILA HAWATOKEI MDIO MAANA UNAONA TUNAHTAJ MSAADA
 
Mimi pia sijaona biashara hapo, yani uwekeze 34.5M (pikipiki 15) kisha upate faida ya 45K per day?

Anyways kila mtu na maisha yake na namna anavyoona inafaa.
Harafu mwisho Mali inakuwa sio yake bora ujenge hata apartment unakusanya Kodi na Mali inabaki yako unaweza hata kukopea
 
Harafu mwisho Mali inakuwa sio yake bora ujenge hata apartment unakusanya Kodi na Mali inabaki yako unaweza hata kukopea
Kuna kitu hapa watu wanashindwa kuelewa Sina mtaji Wa 34.5 Millions, nimesema nilianza na mtaji Wa 9 Millions Kwa kuanza na Pikipiki 4 tu mpka kufika sasa zipo zaidi ya Pikipiki 15.

Mtaji wangu ni 9 Millions + 30% ya Mshahara wangu Kila mwezi mpka kufika hatua hii Kwa muda wa miezi 13 mpka Leo hii.

Sasahivi zimeongezeka Tena maana plan yangu ni Kila mwezi naongeza Pikipiki mbili mpya au USED.
[emoji28][emoji28]
 
Nakushauri ukitaka kufanya jambo lolote

Fanya utafiti wako ukiona limekaa sawa fanya acha kutafuta ushauri kila sehem...

Hkuna kitu ambacho hakina changamoto...ukitaka kufanya fanya bila kuqngalia chochote.....
Shukrani bro, umetoa ushauri Kwa watu wengi zaidi kwamba maishani unachoona ni FAIDA kwako na kipo sawa fanya usimuige mtu mwingine.
 
Mimi pia sijaona biashara hapo, yani uwekeze 34.5M (pikipiki 15) kisha upate faida ya 45K per day?

Anyways kila mtu na maisha yake na namna anavyoona inafaa.
Kuna kitu hapa watu wanashindwa kuelewa Sina mtaji Wa 34.5 Millions, nimesema nilianza na mtaji Wa 9 Millions Kwa kuanza na Pikipiki 4 tu mpka kufika sasa zipo zaidi ya Pikipiki 15.

Mtaji wangu ni 9 Millions + 30% ya Mshahara wangu Kila mwezi mpka kufika hatua hii Kwa muda wa miezi 13 mpka Leo hii.

Statement ya mwisho ndio ya msingi, Kila mmoja afanye anachoona kinampa FAIDA kwake usimuige mtu usiige Biashara kwasabab mwingine anafanya na anafaidika.
 
Chief wapi napata pikipiki used nzuri?
 
Chief wapi napata pikipiki used nzuri?
Pikipiki used zinapatikana maeneo uliyopo, ukitaka Pikipiki USED kirahisi nenda sehemu yoyote ya Gereji hzii sehemu wanazouza spare za Pikipiki hapohapo ukiuliza mtu anayeuza Pikipiki used Utapata wengi tu.

Au fanya kwenda sehemu za vijiwe wanapopaki Pikipiki uliza Kwa mdau yoyote atakwambia anayeuza Pikipiki used. Pikipiki used nzuri zunaanzia 1M hizo hazihitaji marekebisho mengi sana.
 
Wekeza huo mtaji wako upate return isiyo na stress. Mtaji wako voda moja kwa siku mia unakuwa umerudi.
 
Sawa, ila jiweke kwenye risk kubwa.

Vijana ni wachache waaminifu.

Uwe tayari kwenda serikali za mitaa na polisi kila mwezi.

Mwisho utaiita ni biashara chechefu
 
Unaenda Kwa Mjumbe au Mwenyekiti wa anayepewa Pikipiki ya Mkataba (Makazi yake rasmi) ni lazima wao wamtambue na Kisha ndio waweke Saini ya Mkataba na mashahidi wake wakiwepo.
na mjumbe naye anaachiwa hela? Hiyo imesomeka kwenye matumizi? Bima, matengenezo etc yanakuwa juu ya nani?
 
Kuna ushuhuda hapa:

Sasa kweli yaani pikipiki 15 ni sawa na milioni 34.5 unaona faida ya 49,500 kwa siku ni sawa kweli?!!Hapanaaa hiyo kwa hesabu za kibiashara ni hakuna kitu hapo!!
Mkuu hebu tupe mfano wa biashara mbadala kwa mtaji wa 34.5m ambayo inaweza kuzalisha faida kubwa zaidi ya hiyo 49.5k kwa siku?
 
Mkuu hebu tupe mfano wa biashara mbadala kwa mtaji wa 34.5m ambayo inaweza kuzalisha faida kubwa zaidi ya hiyo 49.5k kwa siku?
Nakupa mifano ya biashara mbili tu,biashara ya mchele kwa mtaji huo unaweza pata tani 25,ambazo zikakuingizia NET PROFIT ya milioni 5 ndani ya wiki moja hadi nne kutegemea na soko unalopeleka.Nyingine ni ya viazi mlivingo kwa mtaji huo unaweza pata gunia 400 au zaidi kutegemea na walati,,ambazo NET PROFIT kwa gunia ni wastani wa sh. 3000 ambazo soko likiwa zuri ni siku 2-4 tu.TAFAKARI!!!
 
Mala nyingi mtaji mkubwa hizo ndio faidi zake mfano tani 30 mtaji wake milioni 78 mauzo yake milioni 84 mzunguko huo wiki 2 ukitoa mapato vibalua kodi ya pango kula inaweza bakiwa na sh m 4 kwa mwezi milioni 8 kwa mwaka je?
 
Mala nyingi mtaji mkubwa hizo ndio faidi zake mfano tani 30 mtaji wake milioni 78 mauzo yake milioni 84 mzunguko huo wiki 2 ukitoa mapato vibalua kodi ya pango kula inaweza bakiwa na sh m 4 kwa mwezi milioni 8 kwa mwak
Cjakuelewa mkuu!!kwani mimi hiyo biashara nimeifanya sana,mchele tani 30 nilikuwa naupata kwa wastani wa milioni 30!! Huko mikoani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…