Chukua ushauri wa Peri,
Hiyo ndio hesabu ya siku kwa sasa,na kuhusu eneo hilo anajua Dereva utakaempa,maana huwezi kumpangia kituo.
Pia ujue kwamba anakuwa analala nayo yeye(Sio Kitandani).
Hesabu ni Tsh:7,000 kwa siku na analipa kwa wiki kama anaweza kutunza,ila wapo wengien wanalipa kwa siku ila sio wengi.
Pia wapoa mabao kwa wiki anakupa Tsh:50,000
Hesabu yote hapo Services ni kwa Dereva.
Halafu hakikisha unamuandikisha mkataba kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa akiwa na mdhamini.(usikurupuke kichwa kichwa utakuja kulia)
Hesabu ya Tsh:10,000 kwa siku ili baada ya miezi kumi au mwaka iwe yako ni mfumo umepitwa na wakati na mara nyingi ulikuwa ni kwa pikipiki hizo za Sunlg au tetemesha makalio amabpo bei ya ni kati ya 1,600,000 kama sikosei,maana hesabu ya kuipata hiyo 10,000 kwa siku ni ngum kwa biashara ilivyo kwa sasa na pia itakuwa sio biashara yenye malengo.
Maaana ingekuwa hivyo basi Wenye madaladala nao wangefanya hivyo ili baadae madereva na makondakta yawe yakwao.
Nunua Boxer ndio itakutoa na ndio madereva na abiria pia wanaipenda sana,hii itamsadia Dereva wepesi wa kazi yake na yeye aweze kupata pesa ya kula na kukurejeshea pia ni imara sana na zinadum miaka zaidi ya miwili,hizo nyingine hazipendwi sana,maana zinatetemeka,sasa hadi abiria afike anakoenda akishuka anaona kama ------ yanatetemeka lazima ageuke nyuma aulize je kulikoni au kunamtu anamkobea.Na hata Dereva nae akilala usiku anaona ---- linacheza,kazikweli
Chukua kitu Boxer:Muda wake wa kudum kwa ubora wake ni Miaka miwili.
Ni Bishara nzuri ukipata Dereva mzuri,hakkisha inakuwa na full Bima na dereva unamnunulia helmets na unamuwekea full tank wkas siku ya mwanzo kama mtaji kisha unamkadhi unasuburia hesabu yako.
Mie ninazo kama sita zipo njiani,na changamoto ndio kama hizo,Madereva wengine ndio wengine mpaka mpigiane sim arushe ziko moja au mbili,ilasiku zinaenda hakuna biashara amabayo haina changamoto.
Boxer mpya kwa sasa pamoja na Bima,Helmets,na kama ukimtilia Driver mafuta full tagi inakaribia 2,300,000
Mie Pikipiki zangu huwa nabadiisha kila baada ya miezi sita,nakuwa nauza,kama unapesa ninayo moja imenunuliwa mwaka jana mwezi wa kumi na mbili,nimeishanunua nyingine ku replace hiyo,sasa ile ninanuza ikiwa na full Bima mpaka mwezi wa kumi na mbili.
Hii Hapa lete pesa kisha anza kazi hapo hapo,maana inakila kitu na ilikuwa unapatiwa services kila muda wake muafaka.
Kama unafundi anaweza kujakukusaidi kuangalia.
1.8m tu unasepa nayo(Number C )
Hii Hapa