maroon7 mkuu binafsi sijawahi kuifanya hii biashara lakini ninaomba nitoe input yangu kidogo kwa upande ambao binafasi nimewahi kuishiriki.
Kifupi ni biashara nzuri sana, kikubwa inahitaji ubunifu (creativity) kwa kiasi kikubwa. Lengo kuu la kuifanya hii kazi ni kuongeza ufahamu (awareness) ya huduma ama bidhaa kwa lengo la kuongeza wateja ama mauzo kwa mteja (client) wako. Hii inajumuisha vitu vingi ikiwemo promosheni (promotions), kampeni za kimasoko (marketing campaigns), mashindano (contests) na kadhalika.
Mimi nimewahi kushiriki hii kazi kwenye kampuni chache na hasa kazi yangu ni kubuni mawazo (ideas) na kuziandikia mapendekezo (proposals). Observation nilizoona mimi binafsi nilipofanya kazi kwenye hizi kampuni ni kama ifuatavyo:
1. Uwe umejipanga (Be organized). Kuwa na ofisi nzuri inayojiuza yenyewe. Ipendeze, iwe na mpangilio mzuri na kiofisi na kikazi, ikiwemo uwe na vitendea kazi vyote stahiki.
2. Kuwa na timu nzuri ya wabunifu. (Have a great creative team). Sio lazima uwe umewaajiri, unaweza kuwalipa kwa commission kila unapohitaji ushauri (consultancy) au ingizo/mchango wao (input). Kikubwa mtambue kila mmoja na mheshimu kwa nafasi (role) yake. Marketing inahitaji sana ubunifu ili kuliteka soko.
3. Uwe mbele hatua kadhaa (Be a few steps ahead). Hii biashara inahitaji uwe mchambuzi mzuri sana wa mwenendo (trend) ya vitu vingi hasa vinavyohitaji kufanyiwa marketing. Uwe mwepesi kuona mapengo (gaps) kwenye biashara kiujumla lakini katika upana wa kazi unayotaka kufanya. Uwe na taarifa za kutosha (be well informed) ili unapoingia kazini (field) ufanye kwa uhakika zaidi ili mteja (client) wako aweze kupata matokeo anayotarajia (expected results) kutokana na kazi yako.
Baaad ya hapa kuna kipengele cha KUTAFUTA NA KUPATA KAZI/TENDA. Hapa ni uwezo wako binafsi kupambana ili uweze kupata tenda kwa ajili ya kampuni yako. WOTE niliowafanyia kazi kwenye hizi kampuni wana mtandao mkubwa sana wa wadau wanaofanya hizi kazi. Wanawasiliana kwa karibu sana na Marketing Managers, Procurements Managers na wenye vyeo vinavyoweza kupitisha tenda ama kazi (in English: Decision Makers). Kuwa na kampuni nzuri iliyojipanga halafu tenda hupati itakuwa si jambo zuri.
Binafsi huu ndio mchango wangu mkuu, kiukweli nimeiona ni ni biashara nzuri na ninakutakia heri.