Mkuu sina uzoefu sana ila nimefanya kazi kwenye utalii wa kawaida na hunting safaris kidogo ,niligundua business opportunity moja ambayo wengi hawajaona .Wengi wanapenda kujenga maghorofa ya kifahari sana mjini kama hotels zinazowagharimu billions with payback period ya zaidi ya miaka 50 .Lakini cheap investment with high return .kuna uhaba mkubwa wa accommodation kwenye hifadhi zetu especially Nothern Circuit.Ukiweza kwenda TANAPA ukaongea nao wakakupa mwongozo jinsi ya kuweka semi-luxury camp itakua nzuri sana na utapata wageni wa kutosha.Unahitaji kama hema 10 (double beds) za wageni ambazo on average zinaweza kugharimu kama 4-6 millions/unit (including their poles),then utaweka na furnitures na kufanya plumbing ili liwe self,then ujenge mess ambayo inaweza kukugharimu kama 20 millions maana unaijenga juu ili wanyama waweze kupita chini na wageni waweze kupata park view nzuri.Unaweka na kitchen tent na hema za wafanyakazi.Utahitaji solar na standby generator na-resupply truck ambayo unaweza kukodi mwanzoni,halafu unanunua zile fridge zinazotumia gas . Tatzizo kubwa ni requirements za Tanapa na vibali vingine kama certificate of TFDA na other certifications na vitu vingine vidogo.Then unaweza ku expand biashara yako taratibu.Hii kitu watu wengi hawaijui na wala hawaioni.Wazo sio baya,unajua Overland trucks ni watu waliojitoa saana.
Na wengi pumzika yao huwa kwenye Magari yao unless wameshuka kwa ajili ya shopping tu.
Fanya uchunguzi wa kutosha saana na wa kina saana.Na hali ya usalama kwa sasa sikushauri uanze hii biashara.
Maana idadi yao inapungua,maaana wengi wa South Africa na Wajerumani,ambapo usalama ukiwa duni basi wanatumia ndege.
So,fanya uchunguzi wa kutosha,usije kukuta unalipia kodi tuu bila biashara.Wale jamaa hata kuoga huwa hawataki,asiee wabishi saana wale Watalii wa kwenye Magari.Hahahaha
Wapo ambao smart,ila kuna kipindi ukute wajerumani waliopinda,aisee wavivu hadi kuoga.Sasa kwenye kutumia ndio kabisaa,wanajua hadi bei ya andazi