Sijaelewa unataka kuwa kama wakala wa kununua kutoka kwa watengenezaji na kuuza kwa wafugaji? au unataka kuanzisha/kuproduce brand yako mwenyewe na kuuza.?
Hakuna biashara ambayo hailipi inategemea umetarget vipi soko lako,
wafugaji wapo wengi na kila mfugaji anachakula anachokiamini ktk kulisha kuku wake. Angalia eneo ulipo Je wafugaji wanapendelea kulisha chakula gani na kwanini? Fanya survey ya eneo lako la biashara ndipo uanzie hapo.