Biashara ya Chakula cha Mifugo

Biashara ya Chakula cha Mifugo

Mambo Jambo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2008
Posts
1,100
Reaction score
82
Wakuu habari zenu,

Kwa muda nimekuwa na hamu ya kuanzisha biashara ya Chakula cha mifugo, kwa ajili ya wafugaji. Lakini mbali na chakula nitauza vifaa vya ufugaji na nitakuwa wakala wa vifaranga vya kuku wa kisasa, kienyeji na kwale na nitakuwa natoa huduma ya utotoleshaji vifaranga.

Chakula nitakachouza ni pamoja na mahindi, dengu, mashudu ya alizeti, mashudu ya pamba etc, na vile vile nitakuwa wakala wa kuuza chakula cha kuku wa kisasa laani layers na broilers. Hii ni plan yangu ya muda mfupi lakini baada ya muda wa mwaka mmoja nataka nianze kupack chakula changu mwenyewe, nadhani by then nitakuwa nimeshanunua mashine ya kutayarishia vyakula vya mifugo na vifaa vya packaging.

Naomba mwana JF mwenye uzoefu na biashara hii anipe ushauri wa nini cha kufanya, wapi naweza kupata bidhaa hizi kwa bei nzuri itakayo niletea faida nzuri. Na changamoto zake kwa ujumla.

Location ninayo na ni nje ya mji, kwa hiyo kwa ufupi kodi ya pango ninayo, budget ya promotion ninayo, Bei ya kununua bidhaa ninayo na Bei za kuuzia ninazo tayari.

Naombeni ushauri wenu.

Wasalaam Mambo Jambo, Dar es Salaam
 
Wazo zuri mdau, pigana asibuhi

Asante kaka, nilishalipia pango na sasa natengeneza promotion materials, kama signboards, leaflets, flyers etc.

Naamini wazoefu wa biasharahii watanipa ushauri wa kutosha
 
mimi ntakusupply mashudu kama wataka kuanzi tani 25
 
Wakuu habari zenu,

Kwa muda nimekuwa na hamu ya kuanzisha biashara ya Chakula cha mifugo, kwa ajili ya wafugaji. Lakini mbali na chakula nitauza vifaa vya ufugaji na nitakuwa wakala wa vifaranga vya kuku wa kisasa, kienyeji na kwale na nitakuwa natoa huduma ya utotoleshaji vifaranga.

Chakula nitakachouza ni pamoja na mahindi, dengu, mashudu ya alizeti, mashudu ya pamba etc, na vile vile nitakuwa wakala wa kuuza chakula cha kuku wa kisasa laani layers na broilers. Hii ni plan yangu ya muda mfupi lakini baada ya muda wa mwaka mmoja nataka nianze kupack chakula changu mwenyewe, nadhani by then nitakuwa nimeshanunua mashine ya kutayarishia vyakula vya mifugo na vifaa vya packaging.

Naomba mwana JF mwenye uzoefu na biashara hii anipe ushauri wa nini cha kufanya, wapi naweza kupata bidhaa hizi kwa bei nzuri itakayo niletea faida nzuri. Na changamoto zake kwa ujumla.

Location ninayo na ni nje ya mji, kwa hiyo kwa ufupi kodi ya pango ninayo, budget ya promotion ninayo, Bei ya kununua bidhaa ninayo na Bei za kuuzia ninazo tayari.

Naombeni ushauri wenu.

Wasalaam Mambo Jambo, Dar es Salaam

Mambo Jambo Hi,

Hii ni biashara nzuri sana kuna jamaa yangu aliianza kimzaha mzaha lakini sasa hivi ni miongoni mwa suppliers wakubwa wa Chakula cha mifugo Jijini Mwanza, Na yeye alianza kama wewe alianza na kuuza mahindi, mtama, uwele, mashudu ya pamba, ya alizeti, dona ya mbwa, dagaa, unga wa mapank n.k lakini baada ya miaka kadhaa ameanzisha kiwanda cha kutengeneza chalula cha mifugo, na market share aliyonayo ni kubwa sana, sasa zingatia haya:-
1. Kwa kuwa uko Dar nunua bidhaa zako mikoani, kwa mfano mahindi, mtama na uwele nunua Dodoma, upande wa mashudu ya alizeti nunua Singida, mashudu ya pamba sinyanga, dagaa wa mwanza agiza Mwanza, mabaki ya samaki chukua bagamoyo....vitu kama pumba, chokaa, mifupa unaweza nunua dar

2. Fanya Door to Door sell kwa wafugaji walio karibu na maeneo ya biashara yako, kuwa mwema na mwaminifu kwao, weka mtaalamu wa mifugo na kilimo dukani kwa ajili ya ushauri kwa wafugaji.

3. Weka duka la dawa za mifugo next na duka lako la chakula cha mifugo

Baadaa ya mwaka mmoja tukutane Nyamachobis ili uninunulie moja baridi huku ukinipa mrejesho.
 
Wazo zuri anza kwa kufungua kampuni au jisajili kibiashara kwani kuna fund ziko nje nje kwa miradi kama yako kikubwa uwe umeanza....
 
Wazo zuri anza kwa kufungua kampuni au jisajili kibiashara kwani kuna fund ziko nje nje kwa miradi kama yako kikubwa uwe umeanza....

Mkuu Kasenene habari mkuu,

Nimekutumia PM, tafadhari ipitie
 
Mkuu Elungata heshima mbele, uko mkoa gani, bei zako zikoje mkuu na vipi unagharamia usafiri mpaka store kwangu

usafiri unapolipa mzigo,unalipia na transport ila unalipia hukohuko kwa bank,kisha mzigo unapakiwa na kukukuta huko.,
namba ya gari,leseni ya dreva na kadi ya gari utatumiwa kwa fax,na hivyo utakua na mawasiliao na dreva tangu bado anapakia mzigo mpaka anakufikia....
 
Biashara ya Chakula cha Mifugo inalipa hata zaidi ya ufugaji wenyewe..., Margins za kutosha..

Ila wachanganyaji / watengenezaji wengi wa Bongo wababaishaji tu..., inabidi feed value iwe inapimwa kabisa maabara (protein, Fiber, Carbohydrates n.k.) sio tu kutumia known feed value ya kitu fulani..

Kenya kuna maabara kabisa wanapima na wanahakikisha uchanganyaji na utengenezaji ni wa makini na hakuna contamination, sio unamuuzia mteja anakwenda kuua mifugo yake.....
 
Ni kweli kabisa, hivi ni vitu vinavyotakiwa kufanyiwa kazi ili wafugaji wafuge kwa tija na iwe kweli Ufugaji wa Kibiashara, asante kwa mchango wako
 
Back
Top Bottom