Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Nimelichukuwa wazo lako
 
Jinsi ya kuanzisha biashara ya chips kwa 435,000

Gharama za kudumu
Jiko la chips. 30,000
Jiko la mishikaki 25,000-45,000
Kabati la vioo 200,000
Sahani 10. 15,000
Vikorokoro vya kusaidia kazi 30,000
Ndoo unaweza Tumia za kwako sio lazima Ununue

Gharama za kuendesha biashara

Kodi. 50,000 kila siku pengine 3000
Mkaa 7000
Ndoo ya Viazi 15,000
Kuku 10000
Mafuta 3 litre @14,000
Mayai Trey moja 8000

Usisahau Maji, umeme, pia miundombinu ya sehemu utakapofanyia biashara yako hiyo
 
Asante
 
Kaka na upande huu umepitia pitia kidogo?
Saa ngapi tena
Nimerejea sasa naomba niongee mtazamo wangu na kile ninachofahamu
Biashara ya chakula ni nzuri sana kama una wateja wa uhakika na hakuna ushindani na bei ni nzuri... Unakuwa na target ya siku ama wiki
Lakini sasa kama unapika na huna wateja wa uhakika na bei zako ni hizi bei za mitaani na kuna ushindani utapata tabu sana
Huko kuna ushindani halali na haramu
Huko kuna ushirikina na uchawi
Huko ili kupata faida nzuri unahitaji kufanya dhambi, dhuluma ama ujanjaujanja kama kupata vitu vya wizi, na ambavyo viko chini ya viwango.... Mchele, maharagwe, nyama, kuni mkaa mafuta nknk
Kuepuka hasara inabidi chakula kikibaki usikitupe bali ukizimue siku inayofuata na hata kama kila dalili za kuharibika inabidi kufumba macho tu
Upunjaji wa kipimo cha nia ya kuongeza faida ni mambo yanayofanyika sana....
Sasa kama unataka kufanya hii biashara jiandae na hizi changamoto... Unaweza kufanya halali unafilisika na wenzio wakafanya haramu wanatoboa... Utachagua upande gani? Kazi ni kwako
 
Inamaana nikijikita kwa Mungu na nikafanya haki badi mambo yatakuwa magumu.?
 
Jifunze kulpa kutokana na faida kwa asilimia so mfanyakz wako umwambie labda ntakulpa 30% ya faida ya biashara

So hutoumiza kichwa tatzo mnataja ntakulpa lak1 then bila kuanisha unamlpa kutokana na nn

Alafu hawa binadamu(wafanyakz) wengine sio waamnifu

Kama biashara haina faid automatically hakuna mshahara
 
Chips zinalipa sana..
Kuna ndugu yangu kila siku alikuwa ananipiga misele ya hela nikashauriwa nimfungulie biashara ya chips..

Hivi sasa anapiga hela kwa kwenda front hata kwangu hafiki tena. Ila nikipaki kamkongojo kangu pale kama kawa namuungisha.

Biashara yoyote haitaki anasa ndo maana unashauriwa kuliko umhonge mtu bora umfungulie kitu cha maana huenda atakuombea dua siku moja...
 
Mpwa wangu alianza hiyo biashara Arusha, kijiwe chake kina wateja. Siku hizi hata akija home kwenye misiba anazika na kuondoka. Anasema wateja wakikukosa siku mbili tatu wanahama kijiwe.
 
Hornet kijiwe cha chips umeanza kuongelea mpaka biriani mkuu???
 
Inatakiwa kushika wateja sana
Mpwa wangu alianza hiyo biashara Arusha, kijiwe chake kina wateja. Siku hizi hata akija home kwenye misiba anazika na kuondoka. Anasema wateja wakikukosa siku mbili tatu wanahama kijiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…