Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

Wakuu mnaendeleaje hapo musoma na soko la dagaa. Tupeni updates.
 
Mkuu mbona swali langu umepiga kimya kunijibu kuhusu Uduvi nikiwa Tanga maeneo gani nitapata Uduvi na kwa bei nafuu maana nashinda kwaajili ya mifugo yangu.
Mkuu bado unahitaji uduvi? Je unapatikana wapi?
 
Msimu wa dagaa upoje Tanga?
 
Magoma ndio nimeishi mkuu senta yetu makangara.
Dah nimeikumbuka Korogwe.
 
Jamani poleni na kazi, baada ya kufanya biashara ya dagaa kwa muda fulani kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam nataka nipanue wigo wa kupeleka mkoani Songwe mpakani mwa Tanzania na Zambia (Tunduma)

Lakini kabla sijapata kwanza nilitaka nipate mawasiliano ya watu au wanunuzi wa dagaa kwa bei ya jumla.

Kama upo au unamfahamu INBOX MESSAGE
 
Nipo Mbeya nitume nikakutafutie soko ntakupa majibu.
 
Wa mikoa mingine tukitaka inakuwaje
 
Nitarudi kuelezea vizuri kuhusu hii biashara kesho ngoja nilale kwanza, nimepita huku mida mibaya.
 
Karibu mkuu, leo ndio hii.

UZOEFU WANGU

Wazo lako la kupanua wigo wa kibiashara ni zuri

Nimewahi kuifanya hii biashara miaka 5 iliyopita kwa Dar, haikunipa matunda sana nikaamua kuacha.

Sababu kubwa ilikuwa udalali kama kawaida zilivyobiashara nyingi za Dar.

Sababu ya pili ni soko jinsi unavyonunua na kuuza ni tofauti.

Mwanza utanunua kwa debe ila Dar utauza kwa kilo soko halitambui kipimo cha debe.

Changamoto inakuja kwenye aina ya dagaa na uzito utakaotoa, kuna uwezekano mkubwa sana wakukupoteza mtaji.

Unakonunua unakutana na madalali lazima wakupige unakoenda kuuza pia unakutana na madalali lazima ule nao, hapo unategemea utapata nini? mbaya zaidi uwe mgeni kabisa katika hii biashara na dagaa hauwajui vizuri.

Kwa upande wa Tunduma ndipo ninapopatikana ila sijawahi kuifanya huku, lakini nimewahi kufatilia jinsi soko lilivyo ikohivi;

Tunduma wananunua na kuuza kwa debe kama ilivyo Mza, bei ya sasa sifahamu mpaka niulizie.

Unatafuta mtu wa kufanya nae biashara unamtumia mzigo anauza kisha anakutumia pesa kulingana na makubaliano yenu

Wafanyabiashara wengi huku wanamiliki stoo ila mtaji wa mzigo hawana, wenye mitaji mikubwa wanafata wenyewe na kuwasambazia wenye stoo wasiyokuwa na mtaji kwa mali kauli.

Kwahiyo usiwe na matumaini makubwa sana kwamba utapiga hela kwa muda mfupi sababu tayari kuna watu wameshatengeneza falme zao katika biashara hii, labda uje na mbinu na mawazo mapya.

Biashara ya dagaa hapa haijachangamka sana na wanunuzi wakubwa wa hii bidhaa ni jirani zetu Wazambia na Wakongo, lakini kwa upande wa Wazambia wanapendelea zaidi furu wale samaki wadogo wadogo wanaochambuliwa toka kwenye dagaa nafikiri unawafahamu.

Hivyo kama utakuja angalia soko la furu huko Mwanza na huku Tunduma, lakini ukiweza angalia pia soko la vibambara vya sangara havipo huku.

Aina ya dagaa wenye bei huku ni wale wa nyasi wanatoka Bukoba na wale wa mafuta waliyokaangwa

Kuhusu usafirishaji mwaka 2017 kwa gunia moja la dagaa toka Mwanza mpaka Tunduma ilikuwa 7000 kwasasa sifahamu, Utauliza huko Mwaloni(soko la dagaa) Mwanza.

Mwisho japo siyo kwa umuhimu;

Karibu Tunduma border ya wajanja lango kuu la nchi 8 za SADEC Tanzania.
 
Dagaa wa kukaanga shilingi ngapi bei ya jumla we wa Mwanza naomba jibu
 
Asante kwa mchango mzuri.

Naomba kujua bei ya furu kwa Tunduma.
yaani debe moja la furu linanunuliwaje kwa jumla?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…