Ndugu wapendwa napenda kujuwa kuhusu biashara ya fedha za kigeni (usd/ tshs) zinazofanywa kwenye mipaka yetu hususa Tunduma, nilipanda gari za IT zinazoenda mpakani, ndani ya ile gari kulikuwa na vijana watatu ambao ni watanzania katika kupiga nao story walinieleza wao huja dar toka tunduma mara kadhaa kwa lengo la kubadili dola walizozinunua pale mpakani, nilipojaribu kuwa dadisi waliniambia wao hiyo ni biashara yao na wanapata faida ya kuridhisha kwani hununua dola mpakani na kuja kuuza huku Dar ambako rate yake iko juuu. Je kuna yeyote mwenye ufahamu zaidi mimi binafsi nimepanga kwenda huko Tunduma mwezi November 2018 kwa ajili ya kufahamu zaidi. Aksanteni