Biashara ya FUITS SALAD

Biashara ya FUITS SALAD

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Habari wakuu

Nimeuona uzi hapa jukwaani unaozungumzia biashara ya juisi na matunda kwa ujumla nikaona si vibaya ku-share idea yangu ambayo nimeiona kwa muda mrefu ila imekosa ubunifu mzuri.

Kwa mtu mwenye mtaji mdogo na akawa ana uhakika wa kupata matunda kama mapapai, nanasi, tikiti maji na karanga anaweza kuanzisha biashara ya juisi iliyomiksiwa na kupondwa pondwa waswahili wameozea kuiita “FRUIT” . Huu ni mchanganyiko wa matunda ambayo humenywa na kuchanganywa bila kusagwa lakini hukamuliwa kitu kama ndimu ili kuruhusu yapondeke naturally bila kutumia blender na inakua nusi juisi nusu matunda magumu.

Ni juice inayovutia sana walaji wake maana mtu akiiona tu machoni ni lazima ainunue na akiila lazima aagize nyingine, na kwa kuwa hutumia matunda natural walaji wake huwa ni watu wa rika lolote na huliwa muda wowote.

Ni biashara nzuri sana na yenye mtaji mdogo mno na sidhani kama mtaji wake unazidi hata laki tano(500,000), Maana kikubwa ni kuwa na glasi safi na upatikanaji wa matunda na kijana atakayekuwa anakusaidia kukusanya glasi na kuziosha wakati wewe unawapimia wateja na kukusanya pesa kwenye ki-counter chako.

Juzi nilikua chuo cha D.I.T hapa Dar es Salaam nikamuona jamaa mmoja seems hana elimu kubwa sana wala vifaa advanced sana lakini anapiga pesa nzuri mno, glasi moja anauza tsh 500, na watu wanaichangamkia kweli kweli, jamaa anauza kuanzia asubuhi mpaka usiku tofuti na matunda magumu ambayo wengi hula wakati wa lunch mpaka mida ya usiku.

Nilikadiria mtaji wa jamaa kwa haraka haraka nikaona haufiki hata Tsh 500, 000. na kwa siku anaingiza si chini ya Tsh 200,000 na soko lake ni kubwa na la uhakika sana si tu kwa wanachuo lakini pia kwa wafanyakazi wa maofisi mengi ya hapo Posta na Mnazi Mmoja ambao huchomoka kutafuta “cheap and fast foods”.

Ni suala la ubunifu tu, unaweza ukawa na vyombo vyako vikubwa kadhaa vya kutengeneza na kuhifadhi hii kitu mahala halafu ukawa unawapa vijana wanazungusha mjini kama wanavyofanya hawa jamaa wa juisi za Azam na ukawa unapiga hela ya kutosha tu zaidi ya waniga tai wengi walio maofisini kwa wahindi.

Kazi kwenu
 
hiyo juic naiona sana hapa town ila sijawah kunywa
hivi inahitaji kuwa na ubarid ili iweze kununulika?
 
Buni ingine muache mwenzio apige hela
:angry: Amwache kijana mwenzie "atoke". Hata hivyo ni ushauri mzuri tu kwani watu wanaweza kwenda "kutega" sehemu nyingine na wakapiga hela. Kuiga sio tatizo kwani ndio mfumo wa maisha ulivyo na ni moja ya mbinu ya biashara.Tatizo ni kwenda kujichomeka palepale alipo yule jamaa mkashindania wateja kwa biashara ile ile.
 
Habari wakuu

Nimeuona uzi hapa jukwaani unaozungumzia biashara ya juisi na matunda kwa ujumla nikaona si vibaya ku-share idea yangu ambayo nimeiona kwa muda mrefu ila imekosa ubunifu mzuri.

Kwa mtu mwenye mtaji mdogo na akawa ana uhakika wa kupata matunda kama mapapai, nanasi, tikiti maji na karanga anaweza kuanzisha biashara ya juisi iliyomiksiwa na kupondwa pondwa waswahili wameozea kuiita "FRUIT" . Huu ni mchanganyiko wa matunda ambayo humenywa na kuchanganywa bila kusagwa lakini hukamuliwa kitu kama ndimu ili kuruhusu yapondeke naturally bila kutumia blender na inakua nusi juisi nusu matunda magumu.

Ni juice inayovutia sana walaji wake maana mtu akiiona tu machoni ni lazima ainunue na akiila lazima aagize nyingine, na kwa kuwa hutumia matunda natural walaji wake huwa ni watu wa rika lolote na huliwa muda wowote.

Ni biashara nzuri sana na yenye mtaji mdogo mno na sidhani kama mtaji wake unazidi hata laki tano(500,000), Maana kikubwa ni kuwa na glasi safi na upatikanaji wa matunda na kijana atakayekuwa anakusaidia kukusanya glasi na kuziosha wakati wewe unawapimia wateja na kukusanya pesa kwenye ki-counter chako.

Juzi nilikua chuo cha D.I.T hapa Dar es Salaam nikamuona jamaa mmoja seems hana elimu kubwa sana wala vifaa advanced sana lakini anapiga pesa nzuri mno, glasi moja anauza tsh 500, na watu wanaichangamkia kweli kweli, jamaa anauza kuanzia asubuhi mpaka usiku tofuti na matunda magumu ambayo wengi hula wakati wa lunch mpaka mida ya usiku.

Nilikadiria mtaji wa jamaa kwa haraka haraka nikaona haufiki hata Tsh 500, 000. na kwa siku anaingiza si chini ya Tsh 200,000 na soko lake ni kubwa na la uhakika sana si tu kwa wanachuo lakini pia kwa wafanyakazi wa maofisi mengi ya hapo Posta na Mnazi Mmoja ambao huchomoka kutafuta "cheap and fast foods".

Ni suala la ubunifu tu, unaweza ukawa na vyombo vyako vikubwa kadhaa vya kutengeneza na kuhifadhi hii kitu mahala halafu ukawa unawapa vijana wanazungusha mjini kama wanavyofanya hawa jamaa wa juisi za Azam na ukawa unapiga hela ya kutosha tu zaidi ya waniga tai wengi walio maofisini kwa wahindi.

Kazi kwenu

Nimeipenda mkuu, asante sana.
 
:angry: Amwache kijana mwenzie "atoke". Hata hivyo ni ushauri mzuri tu kwani watu wanaweza kwenda "kutega" sehemu nyingine na wakapiga hela. Kuiga sio tatizo kwani ndio mfumo wa maisha ulivyo na ni moja ya mbinu ya biashara.Tatizo ni kwenda kujichomeka palepale alipo yule jamaa mkashindania wateja kwa biashara ile ile.

Kweli mkuu, huu ushauri mzuri kwa sababu tunajifunza kwa watu waliofanikiwa, unajifunza na wewe unaongeza akili yako mkichwa ila tu usimuharibie mwenzio, kama yeye anauza kariakoo, wewe uza mbezi au ubungo mambo ndivyo yanaenda ndugu zangu. Kuiga siyo shida ila ni njia mojawapo ya kujifunza. Binafsi nimependa na kushukuru kwa aliyeweka hii. Tusiwe waoga.
 
ni kutokana ameshindwa kuelezea vizuri ana kutoa utayarishaji wake mzuri ndio maana unaona lugha gongana
 
Back
Top Bottom