Biashara ya genge ni lazima kuwa na TIN na leseni ya biashara?

Kuna mada hii niliwahi kuileta
Changamoto za biashara na ujasiriamali: Usajili, kodi na ada zake

Unapoanza biashara/ujasiriamali unatakiwa kusajili sehemu husika zinazosimamia biashara/shughuli/huduma/ujasiriamali unaofanya/kutoa. Changamoto ipo katika mitaji ya kuweza kukidhi matakwa. Biashara zetu nyingi zipo ktk kundi la biashara ndogo sana ambazo hata ajira kuajiri japo watu wawili ni ngumu. (Kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kodi kwa mtu anaeanza biashara kuna kijalada cha TRA toleo la Januari 2017 unaweza kupitia kinaelezea vema sana)
 
Kwanza shukrani sana kwa maelezo yaliyoshiba,well ndio naanza na mtaji wangu hauzidi laki tano,na mauzo kwa siku ninavyoona hayazidi labda laki au laki mbili kwa kua naanza nadhani hivyo, na mapato kwa mwaka yanaweza kufika hadi mil 3-4-5 may be nakuendelea ila sidhani yakizidi mil8.sina uhakika.frame nimeshakodisha na ninamalizia maandalizi ya shelf tu.halikadhalika sitaweka bidhaa kwenye vifungashio ambavyo navitoa sokoni au shambani moja kwa moja.nashukuru tena.nimeomba muongozo ili nijue natakiwa kuanzia wapi,ndio lengo kuu na kujua natakiwa kua na kitu gani ili nitimize wajibu kitaifa,asante
 
Kwa ulivyofunguka hv (mtaji, mauzo, mapato) kwa mtazamo na mustakabali wa sasa na baadae wa biashara yk ambayo nikiitazama kwa jicho la maono ya mbali waweza ht kuiboresha kuwa " fresh foodstaffs mini supermarket" sajili biashara yako kikamilifu. Ina maana
1. TIN - TRA
Hp utalipa kodi aina tatu ambazo ni A. Kodi ya makadirio lkn naamini itakuwa ZERO ( 0 hautalipa chochote) 2. Ushuru wa stempu 1% ya thamani ya mkataba wa frem 3. Kodi ya zuio 10% kutokana na mkataba ws frem
2. Afya
Nakushauri kwa kuanza muone Afisa afya wa eneo husika ambapo ukisimama vema uhamie TFDA baada ya kupata ushauri na mwongozo
3. Leseni ya biashara
Nenda ktk halmashauri ya manispaa ya eneo lako uombe baada ya kupata TIN na TAX CLEARANCE CERTIFICATE

ANGALIZO
kama mauzo yako makubwa hvyo chini kidogo ya 100k to 200k kwa siku unatakiwa uwe na mashine ya risiti mkuu (EFD) kwani mauzo ya jumla mil 14 kwa mwaka ni wastani wa mauzo ya sh 38,000+ hv. Kisheria unatakiwa uwape risit za mashine wateja wako
 
heheheee,kwa sasa ukitaja tu EFD mtu anakula kona hujawahi ona,thanks brother and nimekuelewa kabisa.nitafungua na kuanza kufuatilia hayo yote step by step.najua kwa sasa wahusika wanatoa ushirikiano mzuri.bravo bro na ninajua wengi watakua wamefaidika kwa uzi huu.cheers!
 
Ńdio mmbarikiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…