Biashara ya Giza kwenye Usajili wa Taasisi za Dini

Biashara ya Giza kwenye Usajili wa Taasisi za Dini

kasanga70

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
222
Reaction score
515
Kuna mambo hii nchi ukitafakari sn unaweza kukosa majibu. Taasisi husika zinazosajili institution nyeti kama za Dini Ni vijiwe vya kupigia hela tu, waziri yupo miaka nenda Rudi, msajili yupo nk.

Ukienda pale kwa msajili wa Taasisi hizo kwanza unakutana na majimama fulani yanakuchanganya kwa kelele, kinyongo, ugumu wa maelekezo, na njaa nje nje unaziona. Kinachohitajika hapo ni pesa yako tuu. They don't care unaelimu sijui ya theology utajijua mwenyewe.

Pili hakuna document yeyote inayokubalika hadi wakuzalishie wao hiyo document na utoe hela ya maana. Ukimaliza hilo mzunguko unaanza hakuna cha mwanasheria sijui wa msajili wala nini Ni mwendo wa hela tuu.

Picha ya nje tunayooneshwa Ni kwamba serikali ipo serious na usajili wa hizi taasisi kama umekidhi vigezo lkn Ni vituko tu.

Kuna case moja naijua " watu mamekidhi vigezo vyote vya usajili Kila kitu including elimu zao za Dini lkn miaka kumi hadi leo usajili hakuna, matokeo yake taasisi inakufa haiwezi kufanya issue yoyote kimaendeleo becoz hakuna account za benki wala utambulisho wowote na wafadhili wame-withdraw. On the other hand Kuna wahuni tu fulani ndani ya mwaka wana usajili tayari wanaendesha mambo yao.

Wito:
Taasisi za Dini kwa nchi kama Marekani na Ulaya zinapewa uzito mkubwa kama taasisi tanzu zinazoweza kuajili, kusaidia watu kijamii, kuanzisha miradi, nk nk hapa kwetu zinatafsiriwa kama ni tishio la usalama... wakati wanaohusika na usajili wamegeuza maduka.

Ifike wakati Serikali muwe serious jamani Kuna mambo ya aibu Sana huko.

Jibuni barua kwa wakati hatuwapi usajili au tunawapa usajili watu waendelee na harakati nyingine kuliko uhuni unaoendelea wa kutegeana mitego ya hela.
 
Mimi nataka nianzishe dini mkuu, nipate till ya uwakala wa mitandao ya simu, naskia zaka ya Bwana haina tozo.
 
Ndio maana haya makanisa wanayaita ya kiroho yamegeuka vijiwe vya mipasho, kwasababu viongozi eake hawana elimu hitajika (theology).

Wao hukimbilia internet wanaokoteza mambo huko wanaenda kuwadanganya waumini wao, na waumini kwa uelewa mdogo wanaamini wanachoambiwa kwa kudanganywa jamaa amepewa ujumbe na "Roho Mtakatifu".

Kumbe kajiongeza kwa ku google kazi ikaisha ya kuwaridhisha waumini wenye tabia za ushabiki wanaosahau kama wameenda Kanisani kufanya nini.

Kwa ulichoandika, naona tatizo kubwa kwenye hizo ofisi ni ukiritimba, wafanyakazi wanakaa ofisi moja muda mrefu mpaka wanasahau mahitaji na vigezo vya kazi zao wanaanza kufanya kazi kwa mazoea (rushwa).

Dawa ni kuwahamisha waje wapya wenye ari na kazi yao walete mabadiliko stahiki, vinginevyo tutazidi kushuhudia ma Askofu feki wenye tuhuma za ngonona ushirikina kila siku.
 
Uhakiki wa kila miaka 5 umesitishwa
Hakuna Cha uhakiki wala nini. Yaani serikali ndio ina entertain wahuni. Watu serious na miradi yao hawapewi usajili. Ila wajanjawajanja wanaojua kutembeza fedha wana Usajili hata wa taasisi tano na zaidi, same people.
 
Ndio maana haya makanisa wanayaita ya kiroho yamegeuka vijiwe vya mipasho, kwasababu viongozi eake hawana elimu hitajika (theology).

Wao hukimbilia internet wanaokoteza mambo huko wanaenda kuwadanganya waumini wao, na waumini kwa uelewa mdogo wanaamini wanachoambiwa kwa kudanganywa jamaa amepewa ujumbe na "Roho Mtakatifu", kumbe kajiongeza kwa ku google kazi ikaisha.

Kwa ulichoandika, naona tatizo kubwa kwenye hizo ofisi ni ukiritimba, wafanyakazi wanakaa ofisi moja muda mrefu mpaka wanasahau mahitaji na vigezo vya kazi zao wanaanza kufanya kazi kwa mazoea.

Dawa ni kuwahamisha waje wapya wenye ari na kazi yao walete mabadiliko stahiki, vinginevyo tutazidi kushuhudia ma Askofu feki wenye tuhuma za ngonona ushirikina kila siku.
Umemaliza...Kuna watu na taaluma zao wamegeuka kuwa wapiga deal na wasaka rushwa pale
 
Hakuna Cha uhakiki wala nini. Yaani serikali ndio ina entertain wahuni. Watu serious na miradi yao hawapewi usajili. Ila wajanjawajanja wanaojua kutembeza fedha wana Usajili hata wa taasisi tano na zaidi, same people.
Mkono mtupu haulambwi
 
Mbona hili ni easy Sana.

Sepa USA mkuu huko utathaminiwa Sana mbona. Achana na Hawa wenye njaa.

Kuna muda huwa wanasema kuwa don't complain about bad social services but complain that you don't have money.
Since if you've money you'll get good doctors,schools,good private transport,your own investment and not depend on your serikali
 
Mimi nataka nianzishe dini mkuu, nipate till ya uwakala wa mitandao ya simu , naskia zaka ya Bwana haina tozo
Ni vizuri kuwa na adabu na matumizi binafsi ya pesa ya mtu. Mfano mtu kalipwa mshahara kodi zote za serikali kakatwa pesa iliyobaki akipenda kulewa au kuhonga Malaya au kutoa zaka kanisani wewe inakuhusu nini hata akimpa tapeli wewe shida yako nini? Ana uhuru wa kutumia pesa yake vyovyote.

Hela wanazohongwa malaya huwa. Mnaenda kufuata kodi? Haya. Si sahihi kumfuatilia mtu hadi senti yake ya mwisho katumiaje akichangia harusi au msiba au kanisa au padri au mchungaji oooh hazikatwi kodi! !! Mawazo ya kijinga

Kama Unadhani ni rahisi kaanzishe na wewe ni fikra za kijinga zimejengeka vichwani kukata wafuasi uwapige pesa tena watanzania sio rahisi. WATANZANIA sio watu wapanda dini sana ukooni wamemkubali kiongozi wa dini ujue ana kitu sio mchezo
 
Hujanielewa boss, unanshtumu bure!! Umewaza kitu ambacho sijawaza
 
Wakati mataifa yaliyoendelea yanatoa uwezeshi au incentives kwa taasisi za Dini Kila mwaka ili zisife ziendelee kusapoti maendeleo, hapa kwetu Kuna viongozi wanafikiria kuanza kutoza Kodi..kama sio laana Ni nini hii.
 
Sijaelewa ina maana nikitaka kujenga msikiti naenda wizara ya mambo ya ndani au huko ni wachungaji tu wanaoanzisha makanisa na si misikiti
 
sijaelewa ina maana nikitaka kujenga msikiti naenda wizara ya mambo ya ndani au huko ni wachungaji tu wanaoanzisha makanisa na si misikiti
Msikiti Ni kitu kimojawapo kinachotambulisha imani au Dini ya kiislamu. BUT Kuna taasisi nyingi zinazoweza kusajiliwa ndani ya imani au Dini ya kiislamu mfano. Chuo Cha mafunzo ya Dini ya kiislamu, mfuko wa kusaidia wanyonge au yatima nk wa kiislamu, taasisi ya mikutano ya uongozi ndani ya Dini ya kiislamu nk no sio msikiti pekeake sheikh..
 
Sasa mtumishi na wewe unalalamika kama watu wa ufalme wa dunia, mamlaka ya ufalme wa mbinguni yako wapi hapa sasa?
 
shukran
 
Sasa mtumishi na wewe unalalamika kama watu wa ufalme wa dunia, mamlaka ya ufalme wa mbinguni yako wapi hapa sasa?
Ogopa Sana aliyevaa mwili. Ana uhalali wa kuwepo duniani. Anaweza kuvuruga na kutumiwa kuharibu mipango mizuri ya ufalme wa Mungu.
 
Ogopa Sana aliyevaa mwili. Ana uhalali wa kuwepo duniani. Anaweza kuvuruga na kutumiwa kuharibu mipango mizuri ya ufalme wa Mungu.
kweli kabisa, inabidi ufanye kitu cha kiroho zaidi....maana hata kukalia hizo nafasi unakuta yamevaa hirizi viunoni.
 
Back
Top Bottom