Biashara ya Ice Cream Center

Biashara ya Ice Cream Center

Fuqin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2018
Posts
306
Reaction score
625
Natumai mu wazima wadau,

Katika pitapita zangu mitaani nimeona maduka yanauza Ice cream pamoja na snacks za kutafuna na unakuta pamejengwa mazingira mazuri kuna viti na meza nje watu wanatoka sehem mbalimbali wanakuja kuenjoy na familia zao. Mfano kuna magomeni Ice cream center na nyengine nyingi.

Mtaji wake kwenye ml 5 tu nadhani inatosha lakini sijajua faida yake kwa siku unaingiza bei gani let say 50000 kwa siku unaweza kupata? Nataka nijitose huko wadau.

Pia, soma: Biashara ya kutengeneza na kuuza "Askrimu" (Ice Lollies)
 
Unajua wenzetu jamii ya zanzibar wana utamafuni wa kutopika jioni, jioni wengi hupenda kula out na familia zao au wapenzi wao, sasa hapo issue ni location angalia maeneo yenye Waarabu, Wahindi, Wazanzibari wengi, Ilala, Magomeni, Kisutu, Manzese, Tandika, ongea na watu wa azam utapiga hela.

Ukifungua hiyo biashara Tabata, Sinza, Kimara imekula kwako, huko ni pombe na kitimoto. Sasa pombe na ice cream haviendani
 
Nadhani pia ukipata eneo karibu na chuo ni vizuri, watoto wazuri wanapenda ice creams, natamani kuifanya hii biashara shida hizo frames karibu na vyuo hazipatikani(occupied)
 
Inawezekana kuwa nzuri ila unahitaji utafiti wa kutosha ili uweze kuingia kwasababu biashara yoyote unayoitaka kuifanya inabidi uifahamu kwanza ndo ufanye
 
Back
Top Bottom